Hivi
ndivyo mandhari nzuri na ya kuvutia ya Daraja la Nyerere lionekanavyo
kwa juu pamoja na flai ova yetu ya kuingilia darajani hapo ndani ya
Wilaya mpya ya Kigamboni.
Sehemu ya mageti ambapo magari yanapaswa kupita wakati wa kufanya malipo yanayotarajiwa kuanza Mei Mosi 2016.
Mhandisi
wa Mradi kutoka kampuni ya China Railway Construction Engineering Group
and Major Bridge Co. Ltd (CRCEG-MBEC JV) Jamal Mruma akitoa ufafanuzi
kwa Wanahabari kuhusiana na ubora wa daraja hilo.
Mhandisi
Mruma alisema kuwa Daraja hilo limejengwa kwa ubora mkubwa na lina
uwezo wa kuhimili uzito zaidi ya tani 50,lakini kwa sasa magari
yanayoruhusiwa ni yale yenye tani kumi kushuka chini,”kwa sasa
tunadhibiti uzito mkubwa kwa sababu kuna baadhi ya maeneo bado
hayajakamilika ikiwemo na barabara ya kuingilia Kigamboni,ambako
hakuwezi kumudu kupitishwa uzito mkubwa”,alibainisha Mhandisi Jamal.
Meneja
Mradi kutoka NSSF,Mhandisi Karim Mataka akizungumzia namna baadhi ya
Madereva ambao wamekuwa wakikiuka taratibu/sheria na alama zilizowekwa
katika daraja hilo kubwa Afrika Mashariki ambalo linatarajiwa kudumu kwa
zaidi ya miaka 100 iwapo litapata matunzo stahiki.
Mhandisi
Karimu amebainisha kuwa magari yanayopaswa kupita hapo kwa sasa yawe
chini ya tani 10,kwa sababu kwa upande wa Kigamboni bado baadhi ya
barabara hazijakamili,hivyo ni vyema Madereva wote wakawa makini.
Daraja
hilo ambalo litaanza kutumika rasmi kwa kulipia Mei Mosi 2016,Mhandisi
Karimu amewataka Watanzania kulinda miundo mbinu ya daraja hilo ikiwemo
kutii sheria zote za Daraja hilo ili kuepuka kusababisha uharibifu wa
aina yoyote ile,kwa sababu limejengwa kwa gharama kubwa na linahitaji
matunzo.
Mhandisi
alibainisha pia kuwa Daraja hilo la Kigamboni ambalo lilizinduliwa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli na
kulibatiza jina la Daraja la Nyerere limejengwa kwa ufadhili wa Serikali
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Shirika la Hifadhi ya Jamii
(NSSF)
Moja ya Lori likikatiza darajani hapo kwa kukiuka taratibu na sheria za Daraja hilo.
Muonekano
wa Daraja la Mwal Nyerere kama lionekanavyo kwa mbaali kidogo
unapoelekea kwenye mageti ya kutokea upande wa pili wa Kigamboni.Daraja
hilo limerahisisha usafiri wa kutoka Kigamboni mpaka kati kati ya jiji
la Dar.
Sehemu ya muonekano wa daraja hilo linapokatiza mkondo wa bahari
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni