NDEGE MBILI ZAGONGANA KATIKA UWANJA WA NDEGE JIJINI JAKARTA

Ndege mbili zimegongana katika uwanja wa ndege nchini Indonesia katika Jiji la Jakarta, na kupelekea bawa la ndege kuwaka moto.

Ndege ya abiria ya Batik ilikuwa ikijiandaa kuruka wakati bawa lake lilipogonga mkia wa ndege ya TransNusa iliyokuwa karibu na njia ya kurukia.

Mamlaka za nchi hiyo zimesema hakuna mtu aliyejeruhiwa katika ajali hiyo iliyotokea jana usiku, na abiria wote walitoka salama.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni