Mchambuzi
 wa Sera na bajeti wa asasi ya Health Promotion Tanzania (HPT), Bw. 
James Mlali akitoa mafunzo kwa waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na 
Dar es Salaam waliokutanishwa pamoja jijini Mwanza na Maria Stopes 
Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. 
Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali
 mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Waandishi
 wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam waliokutanishwa pamoja 
jijini Mwanza na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia ongezeko la idadi ya 
watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 yaliendana na vitendo 
kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini kujionea ongezeko la idadi
 ya watu.
Waandishi
 wa habari wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam wakifuatilia kwa makini 
mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Maria Stopes Tanzania kuzungumzia 
ongezeko la idadi ya watu na uzazi wa mpango. Mafunzo hayo ya siku 2 
yaliendana na vitendo kwa kutembelea maeneo mbali mbali ya vijijini 
kujionea ongezeko la idadi ya watu.
Mwandishi
 wa wandishi na Muandaaji wa vipindi wa habari wa Redio Free Afrika ya 
Mwanza, Migongo akiuliza swali kwa mwezeshaji wa mafunzo hayo.
Wasimamizi wa Mafunzo hayo kutoka Maria Stopes Tanzania.
Mtaalamu
 wa uzazi wa mpango, Bi. Shida Masumbi akiwaonyesha waandishi wa habari 
wa jiji la Mwanza na Dar es Salaam moja ya njia mojawapo inayotumika 
katika uzazi wa mpango.
Mhadhiri
 wa SJMC- UDSM, Bw. Abdallah Katunzi akitoa mwongozo kwa waandishi wa 
habari juu ya mafunzo waliyoyapata waweze kuyafanyia kazi ipasavyo.
Mwandishi
 wa habari wa Gazeti la Citizen, Bernard Lugongo akiuliza maswali. Picha
 zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog – Mwanza.
……………………………………………………………………………………………………..
Na Cathbert Angelo Kajuna, Mwanza.
ASASI
 ya Health Promotion Tanzania (HPT) inayojishuhulisha na ongezeko la 
idadi ya watu na uzazi wa mpango imeiomba Serikali kuongeza bajeti ya 
uzazi wa mpango ifikie Sh. bilioni sita.
Kauli
 hiyo imetolewa na Mchambuzi wa Sera na bajeti wa asasi hiyo, James 
Mlali wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari wa jiji la Mwanza na Dar
 es Salaam yaliyoandaliwa na Maria Stopes Tanzania kuhusu ongezeko la 
idadi ya watu na uzazi wa mpango.
Alisema
 asilimia 27 ndiyo inayotumia uzazi wa mpango na asilimia 25 wanakosa 
huduma hiyo kutokana na ufinyu wa bajeti inayotengwa na Serikali.
Mlali alisema bajeti ikiwa ndogo hata elimu inakuwa ndogo kutokana na ukosefu wa vitendea kazi.
“Bajeti
 inayotengwa inatakiwa iendane na ongezeko la idadi ya watu kwa 
kuzingatia upatikanaji wa huduma za kijamii ambazo ni elimu,afya, na 
ajira.
“Pia
 ongezeko hili alizingatie hali ya uchumi kwasababu asilimia 42 ya 
watoto wamedumaa akili kutokana na ukosefu wa lishe bora,” alisema 
Mlali.
Mtaalamu
 wa uzazi wa mpango, Shida Masumbi alisema kuna njia tatu za uzazi wa 
mpango ambazo ni njia ya muda mfupi, muda mrefu na njia ya kudumu.
Alisema njia za muda mrefu ni kitanzi, kipandikizi na njiti, njia za muda mfupi ni sindano, vidonge na kondomu.
“Pia ipo njia ya kudumu ya uzazi wa mpango ambayo ni mume na mke kufunga kizazi.
“Baadhi
 ya njia za kisasa za uzazi wa mpango husababisha maudhi kwa kukosa 
hedhi, kuongezeka siku za hedhi au kuona matone madogomadogo ya 
damu,”alisema Masumbi.
Alisema
 pamoja na maudhi hayo lakini kuna faida ambazo ni kuzuia vifo kwa mama 
na mtoto, mama kupumnzika kwa muda mrefu na kujishughulisha na kazi 
nyingine za kimaendeleo.
Masumbi alisema mwitikio wa matumizi ya uzazi wa mpango ni mkubwa na wanaume 300 walijitokeza kufunga kizazi kwa mwaka jana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni