Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiongea wakati wa
uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro iliyokuwa na kaulimbiu “
Weka Mlima Safi, Tunza Mazingira Yakutunze” katika lango la Marangu
mwishoni mwa wiki. Wengine pichani ni Mkurugenzi Mkuu wa TANAPA Allan
Kijazi (kati) na Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita
Loibooki.
Wakurugenzi
kutoka TANAPA wakifuatilia uzinduzi wa Kampeni ya usafi Mlima
Kilimanjaro. Kutoka kulia ni Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango
Mtahiko, Mkurugenzi Utumishi na Utawala Bi. Witness Shoo, Mkurugenzi wa
Mipango Dk. Ezekiel Dembe, Mkurugenzi wa Fedha Nassoro Mndeme na nyuma
yake Mkurugenzi wa Utalii na Masoko Ibrahim Mussa.
Wanafunzi kutoka Chuo cha Taaluma ya Wanyamapori Pasiansi Mwanza nao walishiriki katika kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi Mkuu wa Hifadhi ya Kilimanjaro Betrita Loibooki akiongea wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya Usafi Mlima Kilimanjaro.
Baadhi ya wadau walioshiriki kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiwa katika picha ya
pamoja na watumishi wa TANAPA pamoja na wadau kutoka Kampuni mbalimbali
za mawakala wa utalii kutoka Kilimanjaro na Arusha wanaoshiriki Kampeni
maalum ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Saidi Mecky Sadiki akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Meneja Mawasiliano wa TANAPA Pascal Shelutete akiokota uchafu wa taka ngumu wakati wa kampeni ya usafi Mlima Kilimanjaro.
Mazingira safi yataendelea kuufanya Mlima Kilimanjaro kutiririsha maji kwa wingi zaidi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni