MANDELA YAALIKA WATAFITI KUPELAKA UTAFITI WAO


Na  Mustafa   Leu,Arusha.
TAASISI ya  Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia,barani afrika Nelson  Mandela,Imefungua milango kwa baadhi ya watafiti na wagunduzi wa kisayansi ambao tafiti zao hazijafikishwa kwenye taasisi husika kutokana na sababu mbalimbalii kuwasilisha tafiti zao kwenye taasisi hiyo. 


Hii inakuwa ni taasisi ya kwanza ya Wabobezi wa Sayansi na teknolojia barani afrika kufungua milango kwa  watafiti  kuitumia taasisi hiyo kuwasilisha tafiti na gunduzi zao lengo ni kuwaendeleza kwenye tafiti zao 

 
Makamu mkuu wa taasisi hiyo Profesa Anthony Mshandete,anasema kuwa zipo changamoto mbalimbali ambazo zimechangia baadhi ya watafiti kushindwa kuwasilisha tafiti zao na hivyo matokeo ya tafiti zao kuto tambulika kutokana na changamoto hiyo taasisi imefungua milango  kwa watafiti hao .



 Akizungumza na baadhi ya  wanahabari na watafiti  kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia,(COSTECH,) ofisini kwake kuhusu hatua zinazochukuliwa na taasisi hiyo kuwaendeleza watafiti mbalimbali,Profesa Mshandete, amesema taasisi hiyo inathamini Kazi za utafiti na ugunduzi ili ziweze kuleta maendeleo ya haraka.  


Anasema hiyo ni fursa kwa watafiti nchini ambao walishafanya utafiti na kufanya ugunduzi lakini tafiti zao hawajaziwasilisha kwenye taasisi za kisayansi ili ziweze kutoa matokeo yanayosubiriwa ili zinufaishe  umma. K


Kutokana na changamoto hiyo Taasisi hiyo imeamua kufungua milango na kuwaalika  watafiti waliopo nje ya mfumo  kuwasilisha utafiti na ugunduzi zao na kuwezesha kupiga hatua kubwa ya maendeleo kwenye nyanja ya utafiti.



Amesema watafiti na. wabunifu ni muhimu  katika maisha ya sayansi  kwa kuwa sayansi inaamini katika ugunduzi,utafiti,na namba ambazo hutoa matokeo halisi. 

 Profesa Mshandete,amesema kuwa katika kuendeleza na kuhamasisha maswala ya kutafiti na ugunduzi ,tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH,) imefadhili taasisi hiyo ili kuendeleza na kukuza teknolojia ya sayansi na utafiti nchini



. Anasema taasisi hiyo inawaibua watafiti na wagunduzi wasiofahamika na kuwaweka mbele kutokana na. kutambua na kuthamini shughuli zao lengo ni kuongeza idadi ya  watafiti wawe wengi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni