VIJANA MKOANI ARUSHA WAPEWA SIRI YA MAFANIKIO


Mkuu wa wilayaya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro akizungumza na baadhi ya vijana wa jiji la Arusha wakati akifungua mdahalo wa vijana kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha,Gabriel Fabian Daqarro amefungua mdahalo wa vijana wa jijini Arusha kwaniaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, uliofanyika katika chuo cha ufundi Arusha(ATC),mdahalo ulikuwa na lengo lakutoa elimu kwa vijana juu ya fursa mbalimbali za kiuchumi zilizopo katika Mkoa wa Arusha.

Daqarro aliwahamasisha vijana kujiunga na vikundi mbalimbali vilivyosajiriwa ili waweze kupata mikopo ya serikali itakayowasaida katika shughuli mbalimbali zakuinua uchumi wao badala ya wao kukaa vijiweni nakulalamika hakuna ajira.

“Ni vema vijana mkajiunga kwenye vikundi vya watu 8 hadi 30 na mkavisajiri ili muweze kupata mikopo kutoka serikalini kuliko kukaa vijiweni nakusubiri ajila ziwafuate au kulalamika hakuna ajira”.

lisisitiza kuwa vijana pia watafute fursa kwenye soko la jumuiya ya afrika masharika kwani wakilala wao ndio watageuzwa kuwa soko kwasababu fursa zote zitachukuliwa na wageni.

Pia amewahasa wasipendi urahisi wamaisha kwakutaka mafanikio haraka kwa njia zisizo halali kwani ndio zinawapelekea wajiingize katika biashara harama kama zakuuza na kutumia madawa ya kulevya.

Hata hivyo taasisi mbalimbali nazo ziliweza kuonyesha fursa zilizopo katika taasisi zao ambazo zinawafaa vijana kuwajenga kiuchumi,baadhi yao walikuwa ni Shirika  la maendeleo ya viwanda vidogo (SIDO),Shirikisho la maenyesho ya kilimo(TASO),HAKIKA BANK, Taasisi  yamikopo ya mashine (EFTA),VETA na mashirika yanashughulika na vijana kama DSW, VISION FOR YOUTH (V4Y) na Shirika la kilimo cha mbogamboga,matunda na maua(TAHA).

Akielezea zaidi afisa  maendeleo ya vijana,Japhet Kurwa alisema serikali bado inaendelea kutoa taarifa mbalimbali zinazohusu sera ya vijana kupitia midahalo kama hivyo ili vijana waweze kufahamu fursa zilizopo serikalini na waweze kuzichangamkia.

Hata hivyo aliwataka vijana wao wenyewe wajitaidi kutafuta taarifa sahihi katika ofisi mbalimbali za serikali na hasa ofisi yake iko wazi kwaajili yao hivyo wasijisikie kama wamesahaulika katika jamii bali wao hawatakiwi kulala ila nikukamata kila fursa wanayoiyona mbele yao.

Afisa Maendeleo yaVijana wa Mkoa wa Arusha,Japhet Kurwa akiwakaribisha wajumbe wa mdahalo wa vijana katika ukumbi wa chuo cha ufundi Arusha (ATC).

Baadhi ya watoa mada wakiwa pamoja na mgeni rasmi wa mdahalo wa vijana,Jijini Arusha.

Baadhi ya viongozi wa taasisi mbalimbali zinazojishughulisha na shughuli za vijana na vijana mbalimbali waliohudhulia mdahalo wa vijana.

Mkuu wa wilaya ya Arusha Fabian Daqarro akiwa kwenye picha ya pamoja na wajumbe wa mdahalo wa vijana uliofanyika Jijini Arusha.

MD KAYOMBO AKAGUA ENEO LITAKLOTUMIKA KWA AJILI YA MAONESHO YA NANENANE LA MANISPAA YA UBUNGO LILILOPO MKOANI MOROGORO


Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisisitiza jambo mara baada ya kutembelea Shamba litakaloandaliwa kwa ajili ya Maonesho ya Nanenane lililopo Mkoani Morogoro
Na Mathias Canal, Morogoro

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amefanya ukaguzi wa eneo kwa ajili ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) ili kujiridhisha na kutoa maelekezo ya maandalizi kwa kufyeka majani yaliyopo katika eneo la JKT Mtaa wa Nanenane ikiwa ni hatua za ufanisi kwa ajili ya kuelekea Maonesho ya Nane Nane mwanzoni kwa mwezi Agosti.

Kayombo amesema kuwa lengo kuu la kuzuru kwanza ilikuwa ni kujionea eneo hilo sambamba na kuona hali ya utendaji kazi ili kuanza ufyekaji na kuanza kulima mazao ambayo yanakusudiwa kuoneshwa na Manispaa ya Ubungo.

Amesema kuwa katika utendaji wake amekusudia kwenda mwenyewe Field ili kuona hali ya utendaji ilivyo sio kupelekewa Taarifa pekee kwani kufanya hivyo Ukurugenzi alionao utakuwa hauna maana kama ataishia ofisini.

"Rais ametupa mamlaka makubwa ya kuwatumikia wananchi sasa kama tunakaa ofisi pekee nchi haiwezi kusonga mbele badala yake ili tuweze kuwa na mafanikio katika utendaji pamoja na Kukuza uchumi kupitia sekta mbalimbali ni wazi kwamba tunapaswa kuzuru katika maeneo yote tunayoyaongoza" Alisema Kayombo

MD Kayombo amewapa maelekezo Afisa Kilimo na Afisa Mifugo na Uvuvi kuanza haraka iwezekanavyo usafishaji wa shamba hilo lenye ukubwa wa Mita za Mraba 3600 ili kulima na kupanda mazao kusudiwa kwa ajili ya Maonesho ya Kilimo Nane Nane.

Maelekezo mengine ni pamoja na kununua viuatilifu kwa ajili ya kuua wadudu waharibifu na magonjwa, kuandaa mabango na kuainisha aina mbalimbali za malisho iliyooteshwa na kujenga bwawa la samaki.
 

Kayombo alisema kuwa eneo hilo limenunuliwa na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo kwa ajili ya Maonesho ya Nane Nane ambayo hufanyika kila mwaka kwa lengo la kuwakutanisha wakulima, Wafugaji na wavuvi kwa kuwaelimisha na kuwajengea uwezo wa kutumia teknolojia na mbinu za kuongeza uzalishaji katika eneo la Uvuvi, Kilimo na Ufugaji.

Akizungumzia utekelezaji wa maelekezo yaliyotolewa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Kaimu Afisa Kilimo wa Manispaa ya hiyo Ndg Salim Msuya amesema kuwa wanataraji kuanza kutekeleza hivi karibuni ikiwa ni pamoja na kujenga mabanda ya mifugo na sehemu za kusindika mazao ya mifugo, kuandaa mavazi rasmi kwa ajili ya washiriki wa Maonesho.

Mengine ni kukusanya bidhaa za mazao mbalimbali ya wafugaji, wakulima na wavuvi watakaoshiriki Maonesho hayo ya Kilimo Nane Nane kwa ajili ya kuyapeleka Morogoro.

Sambamba na hayo pia Msuya amesema kuwa maandalizi mengine itakuwa ni kutengeneza matuta ya kuoteshea malisho, Kununua mbolea na kuweka kwenye eneo la malisho ya mifugo, kufunga maji katika eneo la malisho yatakayotumika kwa ajili ya umwagiliaji na mifugo itakayopelekwa wakati wa Maonesho.

Msuya ameeleza kuwa maandalizi mengine itakuwa ni kuandaa mashimo katika matuta ya kuotesha miche, Vipande na Mbegu za malisho pamoja na kutayarisha eneo la kwa kusafisha eneolima na kufanya Layout ya eneo la kuchimba bwawa kwa ajili ya ufugaji samaki.

DKT KEBWE AONGOZA KIKAO CHA MAANDALIZI YA MAONESHO YA KILIMO


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe akizungumza wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki 
Baadhi ya washiriki wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki wakifatilia kikao hicho kwa makini
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akisikiliza kwa makini wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Masharikikilichofanyika Mkoani Morogoro
Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mhe Godwin Gondwe akifatilia kwa makini kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki kilichofanyika Mkoani Morogoro, Kushoto kwake ni Katibu Tawala wa Wilaya ya Ubungo Ndg James Mkumbo
Mkuu wa Wilaya ya Muheza Hajat Mhandisi, Mwanasha Tumbo akichangia jambo wakati wa kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki

Na Mathias Canal, Morogoro

Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe ameongoza kikao cha Kamati kuu ya Tathmini na Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo (Nane Nane) Kanda ya Mashariki inayounganisha Mikoa ya Dar es salaam, Tanga, Pwani na Morogoro.

Kikao hicho kilichokuwa na Agenda sita kimefanyika Katika Ukumbi wa JKT Nane Nane Manispaa ya Morogoro ambapo kwa kauli moja kimepitisha Agenda zote sita ikiwemo kupitia Taarifa ya Tathmini ya Maonesho ya Nane Nane 2016 sawia na Taarifa ya Maandalizi ya Maonesho ya Nane Nane ya mwaka 2017 ambayo Kitaifa yanayotaraji kufanyika Mkoani Morogoro.

Akizungumza wakati Akifungua kikao hicho Dkt Kebwe ameitaka kamati inayoratibu shughuli hizo ya TASO kuweka wazi mapato na matumizi ya fedha wanazozipata kwani kufanya hivyo ni kujenga zaidi uaminifu kwa wananchi na kujihuisha kwa pamoja na wadau mbalimbali ili kukuza uchumi nchini kupitia Kilimo.

Dkt Kebwe alisema kuwa TASO kutofanya hivyo ni njia mojawapo ya kuzifanya Halmashauri zingine kutochangia kwa kuhofia fedha zao kutumika pasina weledi uliokusudiwa.

Sambamba na hayo pia amewasihi wadaiwa sugu kulipa madeni yao haraka iwezekanavyo kwani kufanya hivyo itaongeza ustawi na uimara wa Maandalizi ya Maonesho ya Kilimo na hatimaye Kilele chake kuwa na Tija kwa jamii.

Dkt Kebwe amewapongeza wakurugenzi na Wakuu wa Wilaya waliohudhuria katika kikao hicho ambapo alisema kuwa wanafanya kazi nzuri na kuonyesha ushirikiano imara katika Maandalizi hayo japo amesisitiza kuongezwa kwa jitihada za Maandalizi ili Maonesho hayo yawe na weledi na tija.

Sherehe za Maonesho ya Kilimo Nane Nane hufanyika kwa lengo la kuwakutanisha wakulima, wafugaji, na wavuvi kwa kuwaelimisha watazamaji na hasa wakulima, wafugaji na wavuvi kujifunza na kupata uzoefu wa teknolojia na mbinu zinazotumika kuongeza uzalishaji katika eneo la kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Katika Maonesho hayo mambo muhimu hutawala ikiwa ni pamoja na kuonyesha mazao mbalimbali sambamba na mifugo mbalimbali kwenye mabanda.

Akizungumza na Mtandao wa www.wazo-huru.blogspot.com Mara baada ya kumalizika kwa kikao hicho Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo amewapongeza viongozi wote kwa namna ambavyo wanashiriki kuandaa Maonesho hayo huku akisema kuwa pamoja na Halmashauri ya Ubungo kuwa mpya na inaanza kushiriki katika Maonesho hayo kwa Mara ya kwanza atahakikisha kuwa maonesho yanakuwa na tija katika mabanda yote yanayoendelea kuandaliwa na Maafisa Kilimo, Uvuvi na Mifugaji.

MD Kayombo alisema kuwa kupitia Maonesho ya Kilimo mwaka huu 2017 wananchi watapata fursa ya kujifunza mbinu za ufugaji kwa kutumia mabanda bora, Uchanganyaji wa vyakula vya mifugo na ulishaji, Teknolojia bora ya ufugaji wa samaki wengi katika eneo dogo, Utotoleshaji vifaranga kwa kutumia incubator ya kienyeji na kisasa, Uhamilishaji wa samaki na Ng'ombe na teknolojia Nyinginezo.

Akifunga kikao hicho Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Dkt Kebwe Stephen Kebwe ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa Kikao hicho alizitaja changamoto za maandilizi za Maonesho ya Kilimo kuwa ni pamoja na ucheleweshaji wa michango kutoka kwa wadau mbalimbali pamoja na kuchelewa kuthibitisha mialiko kwa wageni walioalikwa kutembelea Maonesho ya Kilimo Nane Nane.

HAFLA YA KUAPISHWA MAWAZIRI, MABALOZI NA KAMISHNA IKULU DAR ES SALAAM LEO


MAG6
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimuapisha Profesa Palamagamba kabudi baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Sheria na Katiba Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
MAG7
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimkabidhi nyenzo za kazi Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
MAG5
Viongozi walioapishwa wakila kiapo cha Maadili ya Viongozi wa Umma Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017. Kutoka kushoto ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa Palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
MAG1
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari wa vyombo mbalimbali baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
MAG2
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan, na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na waapishwa baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017. Waapieshwa hao ni Mhe Jaji Stella Esther Mugasha ambaye ameapishwa kuwa kamishna wa Tume ya Mahakama, Mhe Sylvester Mabumba (Balozi wa Tanzania nchini Oman), Mhe Job Masima (Balozi wa Tanzania nchini Israel), Mhe. Dkt Abdallah Possi (Balozi wa Tanzania nchini Ujerumani), Mhe Profesa palamagamba Kabudi (Waziri wa sheria na katiba) na Dkt Harrison Mwakyembe, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

MAG3
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akimpongeza Dkt. Harrison Mwakyembe baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, huku Waziri mpya wa Sheria na katiba Profesa palamagamba kabudi akiwa pembeni baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017
MAG4
MAG8
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiongea na wanahabari wa vyombo mbalimbali baada ya kuhitimisha hafla ya kuwaapisha mawaziri, mabalozi na Kamishna Ikulu jijini Dar es salaam leo Machi 24, 2017

RAIS TRUMP AKERWA NA MKWEWE NA BINTI YAKE KUWA MAPUMZIKONI WAKATI HUU MUHIMU


Rais Donald Trump ameripotiwa kukasirishwa na kitendo cha mkwewe ambaye ni mshauri wake mwandamizi pamoja na binti yake kuwa katika mapumziko wakati wa kura muhimu ya ya muswada wake wa afya.

Binti yake huyo Ivanka Trump na mumewe Jared Kushner wapo huko Aspen pamoja na watoto wao wakifurahia mapumziko yao kwa kucheza mchezo wa kuteleza kwenye barafu, wakati wa maamuzi muhimu ya muswada huo.

Muswada huo wa afya wa Marekani, umeshindwa kupita katika baraza la Congress licha ya kuwa na wawakilishi wengi wa Republican, ambapo Spika Paul Ryan alilazimika kuuondoa jana.
                    Ivanka Trump akiwa na mumewe Jared Kushner mapumzikoni huko Aspen
           Ivanka Trump na mumewe Jared Kushner wakiteleza kwenye barafu huko Aspen

MASAUNI AWATAKA WANANCHI WAISHIO MPAKANI MWA TANZANIA NA MSUMBIJI KUFUATA SHERIA ZA UHAMIAJI, ATEMBELEA KIWANDACHA KUCHAKATA GESI ASILIA MADIMBA, AAGIZA UJENZI WA KITUO CHA POLISI



UN1
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akimsikiliza Meneja wa Kiwanda cha Kuchakata Gesi Asilia Madimba wa Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), mkoani Mtwara, Mhandisi Sultan Pwaga, wakati Naibu Waziri huyo alipofanya ziara kiwandani hapo kuangalia jinsi gesi inavyozalishwa. Hata hivyo, Masauni alitoa ahadi, Jeshi lake litafanya taratibu kwa kushirikiana na Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda (katikati) pamoja na TPDC kufanikisha uwepo wa Kituo cha Polisi kama walivyoomba uongozi wa Kiwanda hicho kwa ajili ya kuimarisha ulinzi kiwandani hapo pamoja na wananchi waishio jirani na kiwanda hicho. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
UN2
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni(kulia) akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Masauni aliwataka wananchi hao kudumisha amani mpakani hapo pamoja na kufuata sheria za uhamiaji za nchini pamoja na za Uhamiaji Msumbiji endapo watahitaji kuvuka mpaka huo. Masauni baada ya kukagua mpaka huo aliwataka maafisa wakekuimairisha ulinzi zaidi mpakani hapo. Wapili kulia ni Afisa Uhamiaji Mkoa wa Mtwara, Rose Mhagama.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
UN3
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati) akiiangalia moja ya nyumba za askari wa Jeshi la Magereza ambazo zinahitaji marekebisho katika Gereza Lilungu mkoani Mtwara. Kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa huo, ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda. Kushoto ni Mkuu wa Jeshi hilo mkoani humo, Ismail Mlawa.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
UN4
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (wapili kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya kuhitimisha ziara yake kukagua mpaka wa Tanzania na Msumbiji uliopo katika Kijiji cha Kilambo, mkoani Mtwara. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Mtwara, Evod Mmanda. Wapili kulia ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama, na Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa huo, Neema Mwanga. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
UN5
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akiwapa maelekezo maafisa wake wakati alipokuwa Mto Ruvuma, Kijiji cha Kilambo kilichopo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji, mkoani Mtwara.Wapili kushoto ni Afisa Uhamiaji mkoa huo, Rose Mhagama, na anayefuata ni Mkuu wa Jeshi la Polisi mkoa huo, Neema Mwanga.Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
UN6
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kushoto) akikaribishwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Mtwara, Ismail Mlawa kwa ajili ya kwenda kukagua nyumba za askari Magereza wa Gereza Lilungumkoani humo ambazo zinahitaji marekebisho kutokana na kuharibika. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

POLISI YAIPONGEZA SGA SECURITY KWA KUIMARISHA MAFUNZO KWA ASKARI


Makampuni ya ulinzi yanayofanya shughuli zake Jijini Dar es Salaam yametakiwa kutoa mafunzo ya kila mara kwa askari wake kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi ili kukabiliana na changamoto za usalama zinazolikumba Jiji hilo kwa sasa.

Rai hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi katika Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni SACP Suzan Kaganda wakati akifunga mafunzo ya siku tano kwa askari 70 wa kampuni ya ulinzi ya SGA Security yaliyofayika katika makao makuu ya kampuni hiyo, Mbezi Beach. Mafunzo haya yaliandaliwa na Polisi Tanzania katika kuimarisha ufanisi wa askari katika makampuni binafsi.

“Natoa rai kwa makampuni mengine ya ulinzi yaliyopo Mkoa wa Kinondoni yaige mfano mzuri kutoka SGA Security kwa kutoa mafunzo kwa watumishi wao ili kuwaongezea maarifa yatakayowawezesha kufanya kazi kwa kujiamini na kwa uhakika,” alisema.

Alisema jeshi la polisi liko tayari kutoa ushirikiano, msaada wa kitaalamu na ushauri pale itakapohitajika huku akiongeza kuwa jeshi hilo pekee haliwezi kumaliza kabisa uhalifu bila kushirikiana na wadau mablimbali yakiwemo makampuni kama SGA Security.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP Suzan Kaganda akikagua gwaride rasmi lililoandaliwa na askari wa SGA Security wakati wa kuhitimisha mafunzo ya siku tano kwa askari 70 wa kampuni hiyo.

“Aidha nawaasa kuzingatia taratibu na sheria za nchi tunapokuwa tukitimiza majukumu yetu ili kazi yetu iwe na tija kwa jamii tunayoihudumia na taifa kwa ujumla,” alisema na kuwaasa askari waliopata mafunzo kuyatumia vizuri kwa manufaa yao na kampuni kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa SGA Security -Tanzania, Eric Sambu, alisema mafunzo hayo ya mara kwa mara yamekuwa na manufaa makubwa kwa kampuni kwani wameweza kuwajengea askari wao uwezo mkubwa hivi kuwafanya wananchi waongeze imani kwao. Zaidi, Mkurungenzi Mtendaji alishukuru Polisi kuanzisha mchakato huu wa kutoa mafunzo wao wenyewe moja kwa moja hii ni ishara kuwa kazi zetu katika makampuni binafsi zinatambuliwa na Polisi wanatuchukulia kama wadau wao katika kuimarisha ulinzi na usalama nchini.

“Tumekuwa tukiendesha mafunzo haya kwa kushirikiana na jeshi la polisi kwani kazi zetu zinafanana kwa kuwa tupo ili kuhakikisha usalama wa wananchi na mali zao,” alisema.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni SACP, Suzan Kaganda akikabidhi cheti kwa mmoja wa maaskari wa SGA Security wakati akifunga mafunzo kwa askari 70 wa kampuni hiyo.

Alisema katika siku tano za mafunzo askari hao waliweza kujifunza mada tofauti kama vile matumizi ya nguvu na silaha za moto, haki za binadamu, polisi jamii, uvunjifu wa haki za binadamu, huduma kwa wateja na uhusiano wa jamii, doria, eneo la tukio, usuluhishi wa migogoro na nguvu ya kukamata.

“Tutaendelea kutoa mafunzo ya aina hii mara kwa mara kwa kuwa tayari tumeona matunda yake ili askari wetu kote nchini katika sehemu ambazo tunafanya kazi waendelee kuwa na uwezo wa kufanya kazi kwa weledi,” alisema.

Kampuni ya SGA ni moja ya makampuni makubwa ya ulinzi Afrika Mashariki huku ikiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 40 katika ukanda huu na imeajiri zaidi ya wafanyakazi 17000 huku ikiwa imewekeza vikamilifu katika rasilimali tofauti za shughuli za ulinzi na usalama.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Kinondoni SACP Suzan Kaganda akipewa maelezo kuhusu chumba cha mawasiliano cha SGA Security kilichopo Mbezi Beach, Dar es Salaam wakati akifunga mafunzo kwa askari 70 wa kampuni hiyo. Kulia ni Mkuu wa Ufundi wa SGA-Tanzania Prochest Peter.
 
SGA Security ni kampuni ya kwanza binafsi kusajiliwa nchini Tanzania mwaka 1984, kama Group Four Security baadae ikajulikana kama Security Group, baada ya zaidi ya miaka 32 ya shughuli na mafanikio Tanzania na 48 Afrika Mashariki, kampuni imeweza mpaka sasa kuajiri wafanyakazi takriban 5,000 nchini Tanzania na zaidi ya 18,500 katika kanda ya Afrika Mashariki, SGA Security ni moja ya waajiri kubwa katika eneo hilo.

SGA Security ina uwakilishi wa kiasi kikubwa sana katika kila eneo la huduma ya usimamizi na usafirishaji wa pesa na vitu vyenye thamani na inatoa huduma hizi kwa zaidi ya Mabenki na Taasisi za Fedha 55 katika eneo la Afrika Mashariki, pia kwenye kutoa huduma za ulinzi kwa takribani mashirika 65 binafsi, kidiplomasia na NGO sekta katika eneo hilo. SGA Security imejikita zaidi pia katika ulinzi shirikishi kupitia teknolojia zaidi za kisasa kama Closed Circuit TV na Access Control, huduma za radio, Tracking ya magari na ufuatiliaji wa mizigo iwapo safarini (RFID).

KAMPUNI YA MAHINDRA KUISAIDIA ZANZIBAR KATIKA MIRADI YA MAENDELEO

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa ili kutoka Kushoto akizungumza na Wafanyabiashara na Wawekezaji wa Mji wa New Delhi Nchini India kwenye Makamo Makuu wa Shirikisho la Viwanda Mjini New Delhi.
Wa kwanza kutoka Kulia ni Mkuu wa shughuli za Kimataifa za Kampuni ya
Mahindra Bwana Arvind Mathew, wa kwanza kutoka Kushoto ni Mjumbe wa
Baraza la Mapinduzi Dr. Sira Ubwa Mamboya na Kushoto ya Balozi Seif
ni Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili Mh. Mihayo Juma
N’hunga.
Mkuu wa shughuli za Kimataifa za Kampuni ya Mahindra Bwana Arvind Mathew Kushoto akibadilishana mawazo na Balozi Seif mara baada ya kumaliza mazungumzo yao
Balozi Seif akizungumza katika kikao cha pamoja mkati ya Ujumbe wake na Wawekezaji na Wafanyabiashara wa Mji wa New Delhi na Majimbo jirani yanayouzunguuka Mji huo makamo Makuu ya Shirikisho la Viwanda la India Mjini New Delhi. Kushoto ya Balozi Seif ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushauri wa Kimataifa wa CII Bwana K.K Kapila na Kulia yake ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya Bibi Asha Ali Abdulla.
Balozi Seif akimzawadia mlango Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushauri wa Kimataifa wa CII Bwana K.K Kapila mara baada ya kumaliza mazungumzo
yao

Picha na – OMPR – ZNZ.


Kampuni ya Kimataifa ya Uhandisi katika utengenezaji wa vyombo vya
Moto ya Mahindra yenye Makao Makuu yake Mjini New Delhi Nchini India
imeamua kuiunga Mkono Zanzibar katika muelekeo wake wa kuimarisha
miradi ya maendelelo.

Mkuu wa shughuli za Kimataifa wa Kampuni hiyo Bwana Arvind Mathew
alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha pamoja kati ya Uongozi wa
Kampuni yake na Ujumbe wa Zanzibar unaoongozwa na Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kilichofanyika Makao Makuu ya
Kampuni hiyo yaliyopo Mjini New Delhi.
Bwana Arvind Mathew alisema kutokana na kukuwa kwa Teknolojia ndani
ya Kamupuni ya Mahindra, Uongozi wa Taasisi hiyo ya Uhandisi Nchini
India hivi sasa umekusudia kuelekeza nguvu zake katika Mataifa rafiki
kwa nia thabiti ya kuona Mataifa hayo hasa yale ya Bara la Afrika
yanakuwa Kiuchumi.
Alisema Mahindra imejipanga kuangalia njia za kusaidia uimarishaji wa
Sekta ya Kilimo kupitia miundombinu imara na vifaa vya Kisasa
vitakavyoongeza nguvu za uzalishaji kwa kundi kubwa la Wakulima katika
mazao ya viungo yenye tija kubwa katika soko la Kitaifa na Kimataifa.
Alisema Wataalamu wa Kampuni ya Mahindra wamekuwa shahidi katika
safari zao za kawaida kwenye Mataifa mbali mbali waliyowekeza miradi
yao ya Kiuchumi kuwaona Wakulima wa maeneo hayo wakiendesha shughuli
zao katika mazingira magumu.
Bwana Arvind Mathew alieleza kwamba wakulima wengi hasa katika Nchi
changa zinazojikita kuendelea wamekosa Taaluma ya kutosha katika
kuimarisha Kilimo chao jambo ambalo wanadiriki kupata kipato kidogo
huku wakitumia nguvu nyingi zaidi wakati wa uzalishaji.
Naye Mkuu wa Kitengo cha Maendeleo ya Biashara cha Kampuni ya Mahindra Kanda ya Afrika Bwana Saurabh Kohli aliueleza Ujumbe wa Zanzibar ulio
mwishoni mwa ziara yake Nchini India kwamba Mahindra imekusudia kuwa
na Mtandao wa Kimataifa katika mfumo wa Uzalishaji katika Nchi mbali
mbali walizowekeza Ulimwenguni.
 
Bwana Saurabh Kohli alisema Mahindra iliyoasisiwa kwama 1945 ikianza
na uzalishaji wa gari aina ya Jeep kwa sasa tayari imeshawekeza katika
Mataifa Mia Moja kwenye nchi mbali mbali Duniani ikiwa na wafanyakazi
wasiopungua Laki 200,000 ikianza na mtaji wa Dola za Kimarekani U$
Bilioni 16.5.
 
Akitoa shukrani kwa niaba ya ujumbe wake Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Seif alisema ushirikiano wa karibu uliopo kati ya Zanzibar
na Kampuni ya Mahindra umetoa mchango mkubwa katika kuwakomboa
Wananchi na hasa Wakulima wa Zanzibar.
 
Alisema Wananhi wa Zanzibar zaidi ya asilimia 70 walioko Vijijini
katika Visiwa vya Unguja na Pemba wanaendesha maisha yao ya kila siku
kwa kutegemea sekta ya Kilimo.
 
Wakati huo huo Ujumbe wa Zanzibar ulikutana kwa mazungumzo na
Wawekezaji pamoja na Wafanyabiashara tofauti wa Mji wa New Delhi na
Majimbo jirani yanayouzunguuka Mji huo yaliyofanyika Makamo Makuu ya
Shirikisho la Viwanda la India { CII }.
 
Katika mazungumao yao Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirikisho hilo
ambae pia ni Mkurugenzi Mkuu wa Ushauri wa Kimataifa wa CII Bwana K.K
Kapila alisema India na Tanzania ikiwemo Zanzibar kwa ujumla zimekuwa
na ushirikiano wa karibu wa Kibiashara uliotiwa saini mnamo mwaka
1974.
 
Bwana Kapila alisema ushirikikano huo unaoendelea kuimarika kila siku
umeibuwa mchango mkubwa wa msaada wa fedha zitakazosaidia uimarishaji
wa huduma za Maji safi na salama katika Mkoa wa Mjini Magharibi
Zanzibar kufuatia ziara ya mwaka jana ya Uongozi wa ngazi ya juu ya
India uliofika Tanzania Mwezi Disemba mwaka 2015.
 
“ Uwepo wa wafanyakazi zaidi ya 10,000 wanaotoka Nchini India
wakifanya kazi Tanzania na Zanzibar kwa ujumla ni uthibitisho wa
ushirikiano uliopo kati ya pande hizo mbili.
 
Naye kwa upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
alisema Zanzibar imeshafungua milango ya uwekezaji kwa makampuni mbali
mbali ndani na nje ya Nchini tokea miaka ya 90.
 
Alisema zipo sekta ambazo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
imeshazijengea uwezo kwenye miundombinu itakayotoa wepesi kwa Taasisi
pamoja na Makampuni yenye nia na maamuzi ya kutaka kuwekeza miradi
yao ya Kiuchumi Visiwani Zanziobar.
 
Balozi Seif aliitaja baadhi ya miradi hiyo kuwa inapatikana katika
sekta ya Afya, Kilimo, Miundombinu, Elimu pamoja na sekta isiyo ya
kiserikali inayotoa ajira kubwa zaidi kwa makundi ya akina mama na
Vijana.


Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar

RAIS MHE. DKT. MAGUFULI AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA BANDARINI NA KUZUIA MAKONTENA 20 YENYE MCHANGA WA MADINI ULIOKUWA USAFIRISHWE NJE YA NCHI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika ziara ya kushtukiza katika Bandari ya Dar es Salaam kufatilia maagizo yake ya kudhibiti vitendo vya udanganyifu vinavyofanywa na wafanyabiashara wanaogiza na kusafirisha mizigo ndani na nje ya nchi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akihesabu makontena 20 yenye mchanga wa madini ambapo ameamuru kontena hizo zisisafirishwe mahali popote
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa maagizo mbalimbali kuhusu makontena 20 (yanayoonekana nyuma) yenye mchanga wa madiniuliokuwa usafirishwe kwenda nje ya nchi ambapo ameagiza Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote.
Makontena 20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na kutoa maagizo mbalimbali kuhusu makontena 20 (yanayoonekana nyuma) yenye mchanga wa madiniuliokuwa usafirishwe kwenda nje ya nchi ambapo ameagiza Kontena hizo zisisafirishwe mahali popote. Makontena 20 yenye mchanga wa madini yakiwa yamezuiwa kusafirishwa nje ya nchi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli mara alipofanya ziara ya kushtukiza katika bandari ya Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akikagua nyaraka mbalimbali zenye maelezo kuhusu makontena ambayo husafirishwa nje ya nchi katika Bandari ya Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia baadhi ya magari yalivyoingizwa nchini na Wafanyabiashara wakubwa kwa njia isiyo halali ya kudai kuwa ni makontena ya mitumba wakati ndani yake wanaficha magari yakifahari wanayoyachanganya na bidhaa zilizochakaa.
\Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na IGP Ernest Mangu mara baada ya kufanya ukaguzi Bandarini hapo. PICHA NA IKULU