MFUKO wa
hifadhi ya wafanyakazi wa serikali za mitaa,LAPF,umeipongeza serikali kwa
kulipa malimbikizo ya madeni ambayo mfuko huo na mingine ilikuwa ikiidai kwa
miaka mingi na hivyo kuathiri usitawi wa mifuko hiyo..
Meneja wa
LAPF kanda ya kaskazini, Rajabu Kinande, amesema hatua ya serikali kulipa
madeni hayo kumeiongezea mifuko ya hifadhi ya jamii uwezo wa kuhudumia
wanachama wao kwa wakati.
Kinande, ameyasema
hayo Marchi 7 jijini Arusha,alipokuwa
akizungumza na vyombo vya habari kwenye kituo cha mikutano ya kimataifa, AICC,
kuelezea hatua ya maandalizi ya mkutano mkuu wa siku mbili wa mwaka wa wadau wa
LAPF.
Amesema
mkutano huo utafunguliwa na Waziri mkuu
wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania,Mh,Majaliwa Kassim Majaliwa,Marchi 9 mwaka
huu ambapo zaidi ya wanachama 1000 wa mfuko huo wanatarajiwa kuhudhuria.
Awali Meneja
Mawasiliano na Masoko wa LAPF,James Mloe, amesema kuwa kwenye mkutano huo
kutawasilishwa mada mbalimbali zikiwemo Uendeshaji wa shughuli za mfuko
huo,Hesabu zilizokaguliwa na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali(CAG)za mwaka 2015/16
ambapo mfuko huo umepata hati safi ya ukaguzi wa hesabu ,UKusanyaji wa michango ulipaji wa mafao kwa wanachama na uwekezaji
,Utawala bora na usimamizi wa uendeshaji
wa mfuko huo na Raslimali fedha .
Amesema siku
ya kwanza ya mkutano huo Marchi 9 kwa kuzingatia kuwa ni siku ya Figo duniani
mfuko umeandaa upimaji wa figo bure kwa wanachama wote ambao utafanywa na
Madaktari bingwa.
.Mloe,amesema siku ya pili ya mkutano huo
Waziri mkuu Kassim Majaliwa atazindua
program mpya ya mikopo kwa wanachama kwa kushirikiana na benki ya CRDB,
iitwayo Maisha popote ambao ni mkopo wa
kwanza kutolewa na mfuko huo.
Amesema
kauli mbiu ya mwaka huu ni kuibua fursa endelevu za ajira kwa maendeleo endelevu kwa watanzania.
Kuhusu uwekezaji
kwenye viwanda,Mloe, amesema kuwa LAPF, imeweka
mitaji kwenye viwanda ambako
tayari wameweka hisa zao .
Amesema kuwa
LAPF,haiwezi kujenga viwanda na kuvisimamia uendeshaji wake bali itaweka mitaji
na kusisitiza kuwa LAPF itabakia kwenye jukumu lake la msingi la kulinda
michango ya wanachama wake.
Mwisho .
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni