Ubalozi wa Kuwait nchini umekabidhi visima vinne katika shule za msingi Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Shule za Msingi zilizopata visima hivyo ni Yombo, Umoja , Mwale pamoja na Bwawani. Akizungumza wakati wa kukabidhi visima hivyo, Balozi wa Kuwait , Jasem Al-Najem amesema kuwa wanatambua umuhimu wa maji ndiyo maana wameona umuhimu wa visima hivyo katika shule hizo.
Amesema wataendelea kutoa misaada hiyo kutokana na mahitaji yaliyopo katika jamii kutokana na ushirikiano uliopo kati ya Tanzania na Kuwait.
Al-Najem amesema kuwa wameweza kuchimba visima 16 vyenye thamani ya Dola za Kimarekani 63,000 na watu wengine waweze kujitokeza kusaidia jitihada mbalimbali.
Ubalozi huo pia umekabidhi dawa za binadamu katika Hospitali ya Amana zenye thamani sh.milioni tatu.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akizundua kisima cha maji safi katika shule ya Msingi Yombo jijini Dar es Salaam, Kulia ni Naibu Mkurugenzi wa Red Cresene , Anwari Abdallah Al-Hasawi.Picha na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem kushoto na Naibu Mkurugenzi wa Red Cresene , Anwari Abdallah Al-Hasawi wakinywa maji mara baada kuzindua kisima katika shule ya msingi Yombo, jijini Dar es Salaam.
Afisa Elimu, Elimu ya Watu Wazima wa Manispaa ya Ilala , Hamisi Mlangala akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa visima ambapo alishukuru msaada huo.
Balozi wa Kuwait nchini, Jasem Al-Najem akikabidhi dawa kwa Mganga Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni, jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akitembelea Wodi ya Watoto katika Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Kuwait nchini , Jasem Al-Najem akimsikiliza Mganga Mkuu Msaidizi wa Hospitali ya Amana, Amimu Kilomoni leo jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni