Magari yaliyokuwa yamebeba wajumbe wa kamati hiyo yakiwa yameegeshwa baada ya wananchi kuzuia msafara huo wakishikiza kamati kusikiliza kero walizokuwa nazo.
Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukkeni ,kata ya Harashi wakiwa wamezuia msafara wa kamai ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii iliyofanya ziara kutembelea Pori tengefu la Loliondo kupata hali halisi ya mgogoro uliopo .
Wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii walilazimika kushuka na kuzungumza na wananchi hao.
Wajumbe wa kamati hiyo wa kuzungumza na wananchi wa jamii ya wafugaji katika eneo hilo.
Vijana wa jamii ya wafugaji wakiwa wamebeba silaha za jadi .
Mbunge wa Jimbo la Siha ambaye pi ni jummbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii,Godwin Mollel akizungumza na wananchi wa jamii ya Wafugaji katika kijiji cha Mbukeni baada ya kuzia safara wa kamati hiyo.
Na Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
Wananchi wa jamii ya wafugaji katika kijiji cha Mbukeni,Kata ya Harashi ,tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro jana wamezuia kwa muda msafara wa kamati ya kudumu ya Ardhi,Maliasili na Utalii wakishinikiza kusikilizwa kero zao.
Katika Pori tengefu la Loliondo lililopo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha kumekuwa na mgogoro uliodumu kwa zaidi ya miaka 25 sasa huku suluhu ya utatuzi wa kiini cha mgogoro huo kikitafutiwa ufumbuzi.
Kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi,Maliasili na Utalii imetembelea maeneo mbalimbali ya Pori hilo kwa lengo la kujionea hali halisi kabla ya kutoa tamko juu ya mgogoro huo ambapo ikiwa njiani kuelekea Mamlaka ya Ngorongoro ikakutana na kundi la wafugaji wakiwa wamezuia barabara
Hatua ya wafugaji hao kusimamisha msafara wa kamati inakuja muda mfupi baada ya kamati kufanya kikao na wawakilishi wa wafugaji hao,kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Hotel ya Domel.
Wajumbe wa kamati ya Ardhi,Maliasili na Utalii waliozungumza na Clouds Tv ,Sebastian Kapufi na Dkt Godwin Mollel wamesema hatua ya wafugaji hao kuzuia msafara wa kamati ililenga kuvuruga ziara hiyo.
Wajumbe wa kamati ya kudumu ya Bunge ya Ardhi ,Maliasili na Utalii wakiwemo wataalamu na wanasheria imewasili Loliondo ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhandisi,Atashasta Nditiye na kufanya ziara ya kutembelea eneo lenye ukubwa kilomita 1500 za mraba linalokusudiwa kurejeshwa katika hifadhi .
Eneo hili linatajwa kuwa na vyanzo vingi vya maji yanavyotiririka katika mto Gurumeti unaopita katika Hifadhi ya taifa ya Serengeti ambao ni muhimu kiikolojia kutokana na maji yake kutumiwa na wanyama pori katika hifadhi hiyo.
Mwisho.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni