Mkurugenzi
 wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbass akimkaribisha Naibu Katibu Mkuu 
wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nuru Millao (hayupo 
pichani) wakati wa Kikao Kazi cha Maafisa Mawasiliano Serikalini mapema 
hii leo Mjini Dodoma.
Naibu 
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nuru Millao
 akizungumza na Maafisa Mawasiliano wa Serikali (hawapo pichani) wakati 
wa kikao kazi cha maafisa hao mapema hii leo mjini Dodoma, kulia ni 
Mkurugenzi wa Idara ya Habari Dkt. Hassan Abbass .
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakiendelea na kikao kazi mapema hii leo mjini Dodoma.
Bw. 
Dotto Paul toka Shule Kuu ya Uandishi wa Habari (IJMC) akitoa mada kwa 
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa kikao kazi cha maafisa hao 
(hawapo pichani) mapema hii leo mjini Dodoma.
Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakifuatilia mada wakati wa kikao kazi mapema hii leo mjini Dodoma.
Mwenyekiti
 wa Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) Bw. Theophil Makunga akitoa mada 
kwa Maafisa Mawasiliano wa Serikali wakati wa kikao kazi cha maafisa hao
 (hawapo pichani) mapema hii leo mjini Dodoma.
Afisa 
Mawasiliano toka Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Bw. Innocent 
Mungi akichangia mada wakati wa kikao kazi cha Maafisa Mawasiliano wa 
Serikali mapema hii leo mjini Dodoma.
Picha zote na Eliphace Marwa – Maelezo
………..
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO, Dodoma
Naibu 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo Bibi. Nuru 
Millao amewataka Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini kuuza huduma 
zitolewazo na Wizara au Taasisi husika kwa lengo la kutekeleza shughuli 
za Serikali.
Bibi 
Nuru Millao ameyasema hayo leo mjini Dodoma katika Ukumbi wa Hazina 
ndogo wakati wa Kikoa Kazi cha Maafisa Habari na Mawasiliano Serikalini 
kilicholenga kuwajengea uwezo Maafisa Mawasiliano Serikalini.
“Katika
 kikao hiki tutapata nafasi ya kujadiliana namna bora ya kuboresha 
mawasiliano katika maeneo yetu ya kazi, kuisemea Serikali, kuitendea 
haki Serikali katika kuwasilisha taarifa mbalimbali za Serikali” alisema
 Bibi. Millao.
Kwa 
upande wake Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Bw. 
Dotto Paul alisema kuwa wajibu mkuu wa Maafisa Mawasiliano Serikalini ni
 Kufuatilia kwa ukaribu nini kimeripotiwa kwenye vyombo vya habari kwa 
lengo la kuwa tayari kujibu au kufuatilia habari zinazohusu Serikali.
Bw. 
Paul aliyasema hayo wakati akiwasilisha mada kuhusu wajibu wa Maafisa 
Mawasiliano Serikalini katika kutoa taarifa za Serikali kwa Umma kupitia
 vyombo vya habari na Wajibu wa vyombo vya habari katika kutoa habari za
 Serikali kwa Umma.
Aidha 
alisema kuwa kumekuwa na changamoto mbalimbali za maafisa Mawasiliano 
katika kutimiza wajibu wao ikiwemo upungufu wa mafunzo kuhusu tasnia na 
ujuzi wa kutosha ambapo kuna fursa chache za mafunzo na masomo katika 
kuongeza ujuzi kwa maafisa mawasiliano.
Akisisitiza
 zaidi Bw. Paul alisema kuwa mbali na hayo vyombo vya Habari vina Wajibu
 wa kutoa Habari za Serikali kwa Umma na kuutarifu umma kuhusu mipango, 
shughuli na vipaumbele vya serikali pamoja na utekelezaji wake.
“Vyombo
 vya Habari vinatakiwa kuwa daraja na sauti muhimu kati ya umma na 
serikali kwa kuzingatia maoni, mahitaji ya umma na kuyawasilisha kwa 
walengwa kama taasisi a uviongozi kwa kusikiliza upande wao, na 
kuyaripoti” Alisema Bw. Paul.
Nae 
Bw. Theofil Makunga kutoka Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF) 
akiwasilisha mada kuhusu mtazamo wa Wahariri kwa Maafisa Mawasiliano wa 
Serikali, amewataka Maafisa Mawasiliano kuhakikisha wanasimamia idara 
zao ipasavyo kwa kutoa taarifa sahihi kwani vyombo vya habari 
vinawategemea kwa kiwango kikubwa.
“Mawasiliano
 na mahusiano ya Wahariri na Maafisa Mawasiliano Serikalini yawe ya 
ukaribu na kuelewana ili kuweza kupata taarifa sahihi na kwa upana zaidi
 kuhusu tukio fulani kwa lengo la kuboresha shughuli za Serikali” 
alisema Bwa. Makunga.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni