LEMA:ASEMA MADIWANI WA CHADEMA WAOGA YUPO TAYARI KUWAKANA MBELE YA WANANCHI

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika shule katika viwanja vya Ngarenaro Jijini Arusha Leo.
Wapili kutoka kushoto ni mbunge wa Arusha mjini Godbless Lema ,wakwanza kulia ni mbunge wa Simanjiro James OLemilya akifuatiwa na aliyeko kulia kwake ni Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro,akifuatiwa na Wema Sepetu,na wakwanza kulia ni mwenyekiti wa chadema mkoa wa Arusha Derick Magoma

Mbunge Lema akiwa na Wema Sepetu akisaliamia wananchi wa jiji la Arusha
Mamia ya wananchi waliohudhuria katika mkutano huo  jijini Arusha.

Na,Mahmoud Ahmad ,Arusha.

Mbunge wa Arusha mjini Godbless Jonathan Lema amefanya mkutano wake wa kwanza kwa kuzungumza na wananchi wa Arusha baada ya kutoika rumande alipokuwa ameshikiliwa kwa miezi minne

Akizungumza katika mkutano huo Lema amesema kuwa madiwani wa chama cha Demokrasia na maendeleo Chadema watakao kuwa waoga yupo tayari kuwakana mbele ya wananchi na kama hawawezi kuwa majasiri waachanae na chama hicho. 

Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa chama hicho wakiwemo madiwani wote wa chama hicho katika jiji la Arusha pamoja na wabunge wa simanjiro na yule wa Monduli.

Aidha mbunge huyo amesema kuwa yupo kwenye harakati za kukamisha kukiandika kitabu chake kitakachotoka hivi karibuni chenye historia ya maisha halisi ya wafungwa waliopo gerezani bila hatia,sambamba na wale waliobambikiziwa kesi mbalimbali.

Ameataka madiwani kuwa sambamba na yeye na kuachana na kauli wanayoisema ya kuwa wapo nyuma yake kwa kila kitu anachokifanya .

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni