Rais
wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Anthony Mtaka akikabidhi Bendera
kwa manahodha wa timu ya taifa ya riadha kwa upande wa wanaume,Fabian
Joseph (kushoto) na Magdalena Shauri (kulia)Wengine ni Kaimu Mkurugenzi
wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Nyamakumbati Mafuru (mwenye
miwani) ,Meneja Mawasiliano wa TANAPA,Pascal Shelutete na kushoto ni
Meneja wa timu ya taifa ya riadha Meta Petro.
Raisi
wa Shirikisho la Riadha Tanzania ,Anthony Mtaka akizungumza na
wanariadha 28 wanaoelekea nchini Uganda kwa ajili ya Mashindano ya Dunia
ya Mbio za Nyika wakati wa hafla fupi ya kuwaaga iliyofanyika katika
ofisi za Makao Makuu ya TANAPA jijini Arusha.
Kaimu
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Nyamakumbati
Mafuru akitoa neno kwa wanariadha hao,Shirika la Hifadhi za Taifa ndilo
limedhamini wanariadha hao ambao idadi yao katika ushiriki wa mbio hizo
imevunja rekodi ya tangu mwaka 1991.
Baadhi ya wanariadha watakao iwakilisha nchi katika mashindano hayo yatakayofanyika jumapili hii.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) Whilleam Gidabuday akizungumza wakati wa hafala hiyo.
Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete
akizungumza wakati wa hafla ya kuwaaga wanariadha wa timu ya taifa
iliyoandaliwa na shirika hilo jijini Arusha.
Kikosi
cha wanariadha 28 na viongozi 12 kitakachopeperusha Bendera ya Taifa
nchini Uganda katika Mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika
yatakayofanyika Jumapili hii katika mji wa Entebe.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni