NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
MAHAKAMA ya Tanzania, ina mpango wa kuanzisha Kituo maalum kitakachoshughulikia masuala ya mirathi ili kuweza kusogeza huduma za masuala ya mirathi kwa wananchi, ikiwa ni hatua ya kuwapunguzia gharama za fedha wanazozitumia na muda wanaoutumia.
Kutokana na eneo la mirathi limeonekana kuwa na changamoto nyingi na hivyo kuhitaji mtazamo wa pekee Mahakama inaanzisha, Mpango huo ili kuongeza ufanisi na katika kushughulikia mirathi na mambo ya kifamilia.,
Aidha hatua hiyo, itasaidia kuwawezesha makundi maalum ambayo wanawake na watoto wakiwemo na wasimamizi wa mirathi wanaohitaji huduma hiyo kuendelea kushiriki katika shughuli za maendeleo na kukuza uchumi wa nchi.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mwenyekiti wa Mkutano wa Mashauriano kuhusu uanzishaji Kituo Maalum cha kushughulikia masuala ya mirathi, ambaye ni Msajili ya Mahakama Kuu ya Tanzania,Mhe. Ilvin Mugeta kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya Kurekebisha Sheria,uliopo Jijini Dar es Salaam.
“Tuna mapango wa kuanzisha kituo hicho cha huduma za Mahakama kuhusiana na masuala ya mirathi, ambacho kitakuwa na wadau mbalimbali wa Mahakama ya Tanzania ili kuhakikisha huduma za mirathi zinatolewa kwa wakati bila kupoteza muda na gharama,” alisema Mwenyekiti huyo.
Aliongeza kwamba kituo hicho kitaanzishwa katika jiji la Dar es Salaam, ikiwa ni mradi wa mfano, lakini baadae vitaanzishwa katika mikoa mingine.
Aidha Mhe. Mugeta ambaye pia alikuwa mgeni rasmi katika mkutano huo, alisema kituo hicho, kitaanzishwa katika jiji hilo kwa sababu tatizo hilo, kubwa kwa sababu lina wakazi wengi.
Aliitaja sababu ya kuanzishwa kituo hicho, kimetokana kwamba Mahakama ya Tanzania huwa inapokea maoni 3,000 kila siku kuhusiana na masuala hayo.
“Kituo hicho kitakuwa na huduma za Mahakama za Mwanzo, Wilaya na Mahakama Kuu, ili kuweza kuondoa vipingamizi katika utoaji wa huduma hizo.
Alisema katika kituo hicho, kinatarajiwa kuwa na huduma za utoaji wa vyeti vya kuzaliwa na cheti kifo, huduma za mifuko ya hifadhi ya jamii na kibenki.
Baadhi ya wadau wa mkutano huo, walipendekeza kwamba elimu zaidi itolewe kuhusiana na masuala ya mirathi.
Mkutano huo, ambao umeandaliwa na Mahakama ya Tanzania, umewashirikisha baadhi ya viongozi wa Mahakama na wadau mbalimbali ambao ni Chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, ambayo ni (NSSF), (PSPF), Mamlaka ya Usimamia Mifuko ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Chama cha Mawakili Tanganyika(TLS) na Baraza Kuu la Waislaamu Tanzania(BAKWATA).
caption ya picha
Picha ya Baadhi ya wadau wa Mkutano wa Mashauriano kuhusu uanzishaji Kituo Maalum cha kushughulikia masuala ya mirathi , wakiwa katika picha ya pamoja kwenye ukumbi wa mikutano wa Tume ya Kurekebisha Sheria,uliopo Jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni