EMRE CAN AISAIDIA LIVERPOOL KUIFUNGA BURNLEY


Goli la nne la Emre Can katika msimu huu, limemaliza ugumu wa Burnley kutokufungwa na kuifanya Liverpool kujikita katika nafasi nne za juu za Ligi Kuu ya Uingereza.

Liverpool walikuwa chini ya kiwango chao na walijikuta wakiwa nyuma pale Ashley Barnes alipofunga goli baada ya Matthew Lowton kutoa pasi kali iliyowapita mabeki.

Liverpool ilifunga goli la kusawazisha katika kipindi cha pili kupitia Georginio Wijnaldum, kisha baadaye Can akafunga goli la ushindi.
                                Georginio Wijnaldum akifunga goli la kusawazisha la Liverpool

                    Mjerumani Emre Can akifunga goli la pili na kuipa Liverpool ushindi

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni