BALOZI SEIF AZINDUA NDEGE MAALUM YA UTAFITI WA MAFUTA NA GESI ASILIA

Alisema Rasilmali hiyo endapo itapatikana kufuatia utafiti unaoanza
kufanywa hivi sasa itasaidia kwa kiwango kikubwa kupunguza changamoto
nyingi zinazoikabili Serikali Kuu pamoja na Wananchi kwa ujumla.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa tahadhari hiyo wakati wa hafla maalum ya
uzinduzi wa Ndege itakayofanya Utafiti na hatimae uchimbaji wa
Rasilmali ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar iliyofanyika katika Uwanja
wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume nje kidogo ya Kusini ya Mji
wa Zanzibar.
Alisema yapo Mataifa mengi Duniani yakiwemo yale ya Bara la Afrika
yaliyoanza kuzalisha miradi hiyo kwa matumaini makubwa ya kuimarisha
Uchumi wao lakini hivi sasa zimekuwa na changamoto zaidi za Kiuchumi
hali ambayo Zanzibar na Wananchi wake wanapaswa kuwa makini na kujifunza matukio hayo.
Hata hivyo Balozi Seif alisema safari ya Zanzibar kuelekea kwenye
uchumi Mkuu imeanza mara baada ya Baraza la Wawakilishi Zanzibar
kupitisha Mswaada wa kuanzisha sheria inayoiruhusu Zanzibar kutafuta
na kuchimba mafuta yake yenyewe na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa
Braza la Mainduzi kusaini Sheria hiyo.
Alisema busara za Rais Mstaafu wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa
Tanzania Dr. Jakaya Mrisho Kikwete za kusimamia utaratibu wa kupelekwa
mswada Bungeni zimepelekea suala la mafuta na Gesi Asilia hivi sasa
kutoka katika mambo ya Muungano.
Balozi Seif alifahamisha kwamba Zanzibar na Wananchi wake wamefarajika
na mwanzo mzuri wa hatua za awali za utafiti na baadaye uchimbaji wa
Mafuta na Gesi Asilia ndani ya mipaka yake ya Visiwa vya Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kwamba Serikali ya
Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kushirikiana na Kampuni ya Utafiti na
Uchimbaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya Nchini Ras Al – Khaimah { RAK
GAS } kwa juhudi zake zilizoonyesha nia safi ya kushirikiana na
Zanzibar katika Mradi huo mpya wa Mafuta na Gesi. 
Alisema Rak Gas imekuwa mshirikia mkubwa wa Zanzibar katika harakati
za kuwaondoshea dhiki ya huduma za Maji safi na salama Wananchi wa
Zanzibar ambapo tayari Kampuni hiyo imeshafadhili nuchimbwaji wa
visima 100 Unguja na Pemba.
 
“ Tumeshuhudia juhudi kubwa zinazochukuliwa na Serikali ya Rais Al
–Khaimah Kupitia Kampuni ya Rak Gas katika kuunga mkono harakati za
Kijamii Visiwani Zanzibar ”. Alisema Balozi Seif.
Balozi Seif aliwataka Wananchi wote kutokuwa na hofu kwa ndege
itakayohusika na utafiti wa Mafuta na Gesi katikia maeneo
yanayodhaniwa kuwa na Rasilmali hiyo kwa vile itaruka katika maeneo ya
chini zaidi na kuwataka waendelee na shughuli zao kama kawaida.
 
Mapema Mhandisi Muandamizi wa Kampuni ya Rak Gas kutoka Nchini Ras Al
– Khaimah Dr. Osama Abdd – AAL ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar kwa kuanza kuweka Historia mpya katika muelekeo wake wa
mradi wa Kiuchumi wa Mafuta na Gesi Asilia.
 
Dr. Osama alisema Wananchi wa Zanzibar na ndugu zao wa Ras Al –
Khaimah tayari wamekuwa na uhusiano wa Kihistoria uliopelekea kujenga
ushirikiano zaidi katika uanzishwaji wa utafiti wa Mafuta na Gesi
Asilia Zanzibar.
 
Alisisitiza kwamba utiaji Saini Mkataba wa Utafiti wa Rasilmali hiyo
uliofanywa na Serikali zote mbili Nchini Ras Al – Khaimah karibu miaka
miwiliiliyoita ni uthibitisho wa uhusiano huo wa pande hizo mbili.
Naye Msimamizi wa Kampuni ya Bell Geosace Interrises Limited
inayofanya Utafiti huo Bwana Stephane Kunar alisema ataalamu wa
Taasisi hiyo wako makini katika suala ya uhifadhi wa mazingira wakati
wanapoendesha tafiti zao.
 
Bwana Kunar alisema hatua hiyo inakuja kutokana na uzoefu mkubwa
waliyonao wahandisi hao kwa karibu miaka 70 sasa tokea kuanzishwa
kwake ambapo Barani Afrika kazi hiyo wanaiendeleza kwa zaidi ya miaka
15 sasa.
 
Alisema utafiti wao ambaowanaufanya kwa zaidi ya Mita 100 chini ya
ardhi pamoja na maeneo ya Bahari kwa Afrika umeshafanyikka Afrikka
kwa Nchi ya Botswana Brazil Barani Amerika ya Kusini.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
14/3/2017.

Msimamizi wa Kampuni itakayofanya Utafiti wa
Utafutaji wa Mafuta na Gesi Asilia ya Bell Geospace Inteprises
Limited Bwana Stephane Kunar kushoto akimpatia maelezo Makamu wa Pili
wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Kulia nanma ndege Maalum
itakavyofanya utafiti huo katika maeneo ya Visiwa vya Zanzibar.
Kati kati ni Waziri wa Ardhi, Maji, Nishati na Mazingira mhg. Salama
Aboud Talib, wa nyuma yake ni Katibu Mkuu wake Nd. Ali Khalil Mirza na
Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Ayoub Mohamed Mhmoud.
Balozi Seif akiangalia baadhi ya Mitambo iliyomo
ndani ya Ndege maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited
vitakavyochunguza maeneo yenye daliliza uwepo wa Rasilmali ya Mafuta
Zanzibar

Balozi Seif akijaribu kugusa vifaa vitakavyotumika katika kazi kufanya utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia sehemu zenye dalili ya uwepo wa Mafuta na Gesi Visiwani Zanzibar.
Baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege Maalum ya Kampuni ya Bell Geospace Interprises Limited vitakavyofanya utafiti wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar
Baadhi ya Mitambo iliyomo ndani ya Ndege Maalum ya Kampuni ya Bell  vitakavyofanya utafiti wa Rasilmali ya Mafuta Zanzibar

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni