Polisi nchini Kenya wanachunguza tukio la mtu
mmoja kuuwa na kundi la watu baada ya kunyakua fedha ambazo zinadaiwa
zilitolewa na mwanamuziki, Charles Kanyi aka Jaguar.
Mwanamuziki Jaguar ameshatangaza nia
ya kuwania ubunge katika jimbo la Ziwani, na wakati tukio hilo
alikuwa Ziwani kwenye kampeni na alitoa fedha kwa kundi la vijana.
Kwa mujibu wa mashuhuda na polisi,
kiongozi wa kundi hilo alinyakua fedha hizo na kukimbia na ndipo
wenzake walipomkimbiza na kisha kumpiga hadi kufa.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nairobi,
Japheth Koome, amesema bado wanaendelea na uchunguza tukio hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni