WATAFITI WAOMBA USHIRIKIANO WA JARIBU NA TAASISI ZA FEDHA SERIKALI KUWASOGELEA KUSIKILIZA SHIDA


Prisca Libaga Maelezo ArushaI

Imeelezwa kwamba changamoto za ushirikiano kati ya taasisi za kifedha na serikali zinawafanya wabunifu kutofikia malengo ya kuongeza uzalishaji na kutofikiwa kwa Masoko.

Akiongea na Wanahabari watafiti na wabunifu wa kanda ya kaskazini waliopatiwa mafunzo na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Mkurugenzi wa Imara Tecknoloji Alfed Changula ambao wamebuni mashine ya kupukuchulia mazao ya nafaka.

Anasema kwamba Imara Tecknoloji inajishughulisha na utengenezaji wa mashine za kilimo wamebuni kutengeneza kwaajili ya kuwauzia wakulima ambapo Imara Tech ilianza Mwaka 2019 na uzalishaji rasmi ulianza Mwaka 2020.




Taasisi hiyo imeweza kuzalisha Ajira 37,Saba za moja kwa moja na 30 vibarua hadi Sasa na mawakala 15 ambao wanauza mashine hizo maeneo mbalimbali kanda ya kaskazini Lengo likiwa ni kufikia kanda zote nchini kwa Uzalishaji wa mashine mbalimbali  ikiwemo ya kupukuchulia mazao ya nafaka na mashine nyingine.


Anaeleza kwamba Imara Tech,imekuwa na mafanikio kwa kuuza mashine 400 na kuwafikia wakulima 400 katika maeneo mbalimbali ambapo wanazalisha Ajira kadhaa kwa maeneo waliouza bidhaa hizo


Anabainisha kwamba hadi Sasa bado wanakumbana na changamoto kadha wa kadha ikiwemo ya ugumu wa kuwafikia viongozi wa serikali kuweza kujitangaza kusogeza Maarifa na uelewa sanjari na kutatua baadhi ya changamoto wanazokutana nazo.



Changula Anabainisha baadhi ya changamoto hizo ni ushirikiano mdogo kutoka serikalini na taasisi za kifedha,ruzuku kwa wakulima itakayosaidia kununua mashine ,ongezeko la mara kwa mara kwa bei za bati ambazo zinazalishia mashine hizo.

Aidha anasema kwamba wamekuwa wakikumbana na changamoto kadhaa ikiwemo ushirikiano na taasisi za kifedha kushindwa kuwasaidia wakulima mikopo pindi wanapohitaji mashine hizo.ilhali wao hawakopeshi kutokana na gharama kubwa kwa za vifaa na bidhaa ikiwemo upandaji wa bei za bati mara kwa mara.

"Utakuta wateja wanahitaji mashine hizo ambazo zimewasaidia vijana kuzalisha ajira kwa kujiajiri kwa kufunga kwenye bodaboda Sasa sisi tunaposhindwa kuwakopesha inakuwa changamoto ambapo tunapoongea na taasisi za kifedha bado hawapo teyari kuwadhamini"



Kwa mujibu wa Chengula Wanufaika wa ufadhili wa fedha za  Utafiti na Ubunifu katika Sayansi na Teknolojia wameeleza kunufaika na ufadhili huo kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Ilizowasaidia kuongeza ufanisi katika maeneo hayo ila wameomba ruzuku hizo kuongezwa ili kusaidia kuongeza uzalishaji.

Anasema kwamba katika fedha ya ruzuku kutoka COSTECH waneweza kununua mashine ya kukatia mabati na fedha nyingine kufanya Utafiti wa Masoko na kufanikiwa kuongeza uhitaji wa wakulima wanaotaka kununua mashine hizo.

Wanaiomba Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kuwasaidia kuongeza wigo mpana wa ruzuku sanjari na serikali kuwashika mkono kuweza kuzifikia ndoto zao na kuzishirikisha taasisi za kifedha kuwezesha wakulima kununua mashine hizo ambazo zimekuwa mkombozi kwa wakulima nchini.



"Teknolojia inaposambaa kwa haraka inabadilisha kilimo na kuongeza tija kwa wakulima mashine hizo zinaokoa upotevu wa mazao baada ya mavuno na kuyafanya yawe bora"

Hatahivyo Kituo cha kuhamilisha teknolojia ya zana za kilimo Vijijini, Camartec,kimekuwa ni nguzo ya kutengeneza zana za kilimo na kuziuza kwa wakulima ndani na nje ya nchi ili kurahisisha shughuli za kilimo.

Camartec,Imetoa teknolojia ya uzalishaji zana za kilimo na mashine mbalimbali kwa  taasisi ya Imara tec,iliyowezesha kutengeza mashine mbalimbali na zana za kisasa ambazo zinatumika katika kilimo na kurahisisha uvunaji,kuongeza thamani ya mazao



Kutokana na kuwa ni kisima cha teknolojia Camartec,imeiwezesha kiufundi tasisi ya Imara Tech, kubuni, kusanifu na kutengeneza mashine hizo za kisasa ambazo zinarahisisha shughuli za kilimo  na  kuongezaji thamani ya mazao

Kupitia uwezeshaji huo kutoka Camartec,taasisi ya Imara Tec,imeweza kubuni ,kusanifu na kutengeneza mashine na zana zingine za kilimo na kupata masoko makubwa ya kuuza zana hizo katika nchi za Kenya, Uganda,Rwanda na Burundi

MANDELA YAALIKA WATAFITI KUPELAKA UTAFITI WAO


Na  Mustafa   Leu,Arusha.
TAASISI ya  Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia,barani afrika Nelson  Mandela,Imefungua milango kwa baadhi ya watafiti na wagunduzi wa kisayansi ambao tafiti zao hazijafikishwa kwenye taasisi husika kutokana na sababu mbalimbalii kuwasilisha tafiti zao kwenye taasisi hiyo. 


Hii inakuwa ni taasisi ya kwanza ya Wabobezi wa Sayansi na teknolojia barani afrika kufungua milango kwa  watafiti  kuitumia taasisi hiyo kuwasilisha tafiti na gunduzi zao lengo ni kuwaendeleza kwenye tafiti zao 

 
Makamu mkuu wa taasisi hiyo Profesa Anthony Mshandete,anasema kuwa zipo changamoto mbalimbali ambazo zimechangia baadhi ya watafiti kushindwa kuwasilisha tafiti zao na hivyo matokeo ya tafiti zao kuto tambulika kutokana na changamoto hiyo taasisi imefungua milango  kwa watafiti hao .



 Akizungumza na baadhi ya  wanahabari na watafiti  kutoka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia,(COSTECH,) ofisini kwake kuhusu hatua zinazochukuliwa na taasisi hiyo kuwaendeleza watafiti mbalimbali,Profesa Mshandete, amesema taasisi hiyo inathamini Kazi za utafiti na ugunduzi ili ziweze kuleta maendeleo ya haraka.  


Anasema hiyo ni fursa kwa watafiti nchini ambao walishafanya utafiti na kufanya ugunduzi lakini tafiti zao hawajaziwasilisha kwenye taasisi za kisayansi ili ziweze kutoa matokeo yanayosubiriwa ili zinufaishe  umma. K


Kutokana na changamoto hiyo Taasisi hiyo imeamua kufungua milango na kuwaalika  watafiti waliopo nje ya mfumo  kuwasilisha utafiti na ugunduzi zao na kuwezesha kupiga hatua kubwa ya maendeleo kwenye nyanja ya utafiti.



Amesema watafiti na. wabunifu ni muhimu  katika maisha ya sayansi  kwa kuwa sayansi inaamini katika ugunduzi,utafiti,na namba ambazo hutoa matokeo halisi. 

 Profesa Mshandete,amesema kuwa katika kuendeleza na kuhamasisha maswala ya kutafiti na ugunduzi ,tume ya taifa ya sayansi na teknolojia (COSTECH,) imefadhili taasisi hiyo ili kuendeleza na kukuza teknolojia ya sayansi na utafiti nchini



. Anasema taasisi hiyo inawaibua watafiti na wagunduzi wasiofahamika na kuwaweka mbele kutokana na. kutambua na kuthamini shughuli zao lengo ni kuongeza idadi ya  watafiti wawe wengi