Mawakili wa Serikali kuwa na Chama chao-AG


IMG_4075[1]
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi akitoa mada kuhusu Nafasi na Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wakati  wa mkutano unaoendelea wa Mawakili wa Serikali waliokatika  utumishi wa umma. Pamoja na mambo mengine Dk. Kilangi amesema Mawakili wa Seriakali walio katika utumishi wa umma watakuwa na chama chao.
WIN_20180830_142142 (2) - Copy
Sehemu ya mawakili wa  serikali kutoka wizara mbalimbali, Idara na Taasisi zinazojitegema,  Wakala na Serikali za Mitaa ambao wapo Jijini Dodoma kwa mkutano wao wa siku mbili.
Na Mwandishi Maalum, Dodoma
Mwanasheria Mkuu wa Serikali Dk. Adelardus Kilangi amesema,  anakusudia  kuanzisha Chama cha Wanasheria walio  katika utumishi wa Umma.
Dk. Kilangi ameyaeleza hayo   wakati akiwasilisha mada kuhusu  Nafasi na Majukumu ya Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa  Mawakili wa Serikali walio  katika utumishi wa umma wanaokutana  katika mkutano wao wa siku mbili  unaofanyika katika  ukumbi wa mikutano wa  Chuo cha Mipango Jijini   Dodoma.
Mawakili hao wa Serikali  wapatao mia tisa ( 900) wanatoka  Wizara mbalimbali,  Idara za Serikali, Taasisi na  Mashirika yanayojitegemea, Wakala na Mamlaka za Serikali za Mitaa. Mkutano huo  ambao  ni wa pili kufanyikia ulifunguliwa na  Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma.
Mwanasheria Mkuu wa Serikali amebainisha kwamba, kuanzishwa kwa  Chama hicho ni kwa mujibu wa  Ibara ya 74 ya  Muswaada wa  Sheria ya  Marekebisho  Mbalimbali ( Na.2) 2018  inayoeleza kuwa , “ Mwanasheria Mkuu wa Serikali  anaweza  kuanzisha Chama cha Wanasheri katika Utumishi wa Umma”.
Amewaeleza  Mawakili  wa Serikali kwamba Chama hicho kitakuwa  kinakutana  mara moja kwa mwaka kwaajili ya  kujadili masuala mbalimbali ya kisheria ikiwamo  maendeleo ya taaluma hiyo.
Dk. Kilangi amesema, pamoja  na wanachama wa chama hicho kukutana mara moja kwa mwaka,  Waziri mwenye dhamana na  mambo ya sheria anaweza kuitisha mikutano ya wanasheria waliokatika utumishi wa umma kila anapoona kuna umuhimu wa kufanya hivyo.
Amefafanua zaidi kwa kusema, ripoti ya mikutano ya chama   hicho itawasilishwa kwa Waziri wa Katiba na Sheria na kwamba, Waziri atatunga  Kanuni kuhusu  usimamizi, uongozi, muundo na uendeshaji wa shughuli za chama.
Aidha Mwanasheria Mkuu wa Serikali  amesema kuanzishwa kwa  chama cha Mawakili  wa Serikali walio katika utumishi wa Umma hakutawanyima fursa  mawakili hao ya  kujiunga au kuwa wanachama wa  vyama  vingine vya kitaaluma kikiwamo  Tanganyika law Society ( TLS).
Akizungumzia  kuhusu kuanzishwa kwa   daftari la mawakili wa serikali,  Mwanasheria Mkuu amesema, daftari  hili litaanzishwa kwa mujibu  wa Ibara ya 74 ya  Muswaada wa Sheria ya Marekebisho mbalimbali ( Na. 2) 2018 unaotamka kwamba, “ Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataanzisha Daftari la Mawakili wa Serikali ( Roll of State Attorneys)”.
Amesema daftari hilo likuwa na majina ya mawakili wa serikali kwa kuzingatia ukuu ( seniority ) miongoni mwao na kusisitiza kwamba, hatua hiyo haitaathiri sifa au hadhi  ambayo mtu alikuwa nayo kabla ya kuazishwa kwa  daftari  hilo.
Kuhusu mawakili hao  sasa kutambulika kama  wanasheria wa Serikali ( State Attonerys ) Mwanasheria Mkuu wa Serikali amelitolea ufafanuzi kwa kusema
Kila Afisa Sheria aliyeteuliwa au  kuajiriwa katika Wizara, Idara inayojitegemea, wakala au serikali za mitaa sasa anakuwa wakili wa serikali na kwa sababu hiyo yuko chini ya usimamizi wa Mwanasheria Mkuu wa Serikali isipokuwa  kwa Wanasheria wa Serikali ambao wapo chini ya Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na  Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali.
“Hivyo Afisa huyo anachukuliwa kuwa anafanya kazi na kutekeleza majukumu na  mamlaka ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali katika Wizara zao , Idara zinazojitegemea, wakala wa serikali na Serikali za mitaa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ataweweza kutoa maelekezo ya jumla au maelekezo  mahsusi kwa  mawakili wa  serikali  walio katika utumishi wa umma kuhusu utekelezaji wa majukumu yao ya kisheria.
Akawahimiza wanasheria hao kila mmoja wao kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa bidii, maarifa na ujuzi wake huku akitanguliza maslahi ya taifa lake katika  kila jambo analokishughulikia.
Akahadharisha kwamba,  hatasita kuchukua hatua dhidi ya mtumishi yeyote atakaye kiuka maadili ya  Mawakili katika utumishi wake.
Awali akifungua  Mkutano huo Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa  Ibrahim Juma, amewataka  Mawakili wa Serikali  kutumia njia mbadala ya usuluhi katika baadhi  kesi za madai pale inapobidi   na kufikia usuluhishi nje ya Mahakama.
Jaji Mkuu amesema , ikiwa njia ya usuluhishi nje ya  mahakama  utafanyika, basi  utapunguza  muda wa undeshaji kwa kesi hizo ambazo nyingine huchukua hadi miaka kumi bila kufikia muafaka.
“Niwaombe wanasheria wa Serikali  katika kesi  nyingine za madai pale inapobidi wajaribu sana kulenga kufikia usuluhishi wa nje ya mahakama badala ya kuendesha kesi kwa miaka  hata kumi, kuanzia kesi inapoanza ngazi ya chini hadi kufikia Mahakama ya Rufani” amesema Jaji Mkuu na
Akasisitiza  kwamba, “ Kuna wakati wanasheria wa Serikali wanakiri kwa pembeni, kuwa kesi  wanayoendesha haina nafasi ya kushinda au hata wakishinda gharama hadi  kupata ushindi huyo  ni kubwa. Wanapambana tu kwa sababu Mkuu wa Idara au Kitengo amesema hivyo”.
Akasisitiza kwa kusema. “Hapa ndipo ipo haja ya kujenga Imani ya Mawakili hawa ( wa Serikali) na kuwaruhusu wapate usuluhisho wa mashauri nje ya  mahakama”
Akitoa takwimu za Kituo cha Usuluhishi ( Mediation Centre) cha Mahakama Kuu Dar es Salaam kwa mwaka  jana ( 2017) kinaonyesha kuwa jumla ya mashauri 41 yalisuluhishwa na kituo bila ya kufikishwa Mahakama Kuu kwa ajili ya kusikilizwa na kati ya hizo, ni 10 tu zilikuwa za taasisi ya Umma.

WATAKIWA KUACHA KUTUMIA MAGARI YAO YA DHARURA VIBAYA


JC9A2644
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi akiwa akiwa katika kikao na Viongozi wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Arusha waliofika Ofisini kwake kwa ajili ya kujitambulisha
JC9A2650
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha akiwa katika Picha ya pamoja na viongozi wa Makampuni ya ulinzi Mkoa wa Arusha pamoja na Baadhi ya Maofisa wa Polisi mkoani 
………………………
Na Gasto Kwirini wa Polisi Arusha
Jeshi la Polisi Mkoani hapa limeyaonya baadhi ya Makampuni ya Ulinzi kuacha tabia ya kutumia magari yao ya dharura vibaya kinyume na utaratibu pindi wawapo barabarani.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Ramadhani Ng’anzi wakati akiwakaribisha ofisini kwake  Viongozi wapya wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Arusha waliochaguliwa tarehe 11 Agosti mwaka huu katika Ukumbi wa Maofisa wa Polisi Arusha.
“Kuna baadhi ya Magari ya Makampuni ya Ulinzi yanatumiwa vibaya kwa kigezo cha kuwahi dharura japokuwa wakati mwingine huko waendako hakuna hiyo dharura inayowataka wafanye hivyo. Lakini pia pale kwenye ulazima msitumie magari hayo ya  dharura kwa kubeba vitu haramu  kama vile bhangi”. Alionya kamanda Ng’anzi.
Aidha aliwahakikishia kufuatilia na kuzifanyia kazi changamoto zao hasa za ucheleweshwaji wa utolewaji wa vibali vya umiliki wa silaha, ucheleweshwaji wa utolewaji wa matokeo ya alama za Vidole kwa Askari wapya wanaoajiriwa. Ameyataka Makampuni yenye changamoto hizo kuorodhesha majina yao kupitia viongozi hao, na kuyapeleka ofisini kwake ili aweze kuyafanyia kazi kwa kushirikiana na idara husika na matokeo ya Alama hizo na Vibali hivyo viweze kutolewa haraka na kwa wakati.
Pia amewahaidi kuwasiliana na Ofisi ya Mshauri wa Mgambo Mkoa wa Arusha ili Askari ambao hawakupata mafunzo wayapate kwa awamu huku wakiendelea na majukumu yao. Amewataka Viongozi hao kuorodhesha majina ya Askari hao na kuyapeleka Ofisini kwake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Makampuni ya Ulinzi Mkoa wa Arusha Bwana Daudi Mungi kwa niaba ya Viongozi wenzake, alitoa shukrani kwa Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha kwa ushirikiano wa mara kwa mara wanaondelea kuupata na kuhaidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa Jeshi hilo wakati wote.
Awali akiwakaribisha Viongozi hao, Mkuu wa Operesheni wa Polisi Mkoa wa Arusha Mrakibu Mwandamizi wa Polisi (SSP) Elias Tabana Mwita alisema kwamba ataendeleza ushirikiano uliopo kwa Makampuni ya ulinzi hasa ikizingatia kuwa mchango wa Makampuni hayo ni mkubwa katika kuimarisha ulinzi na usalama katika Mkoa huu. Pia aliwataka kufanya kazi kwa kufuata Sheria na taratibu zinazowaongoza.
Mwenyekiti wa Makampuni ya Ulinzi aliambatana na Viongozi wenzake ambao ni Makamu Mwenyekiti Bwana James Rugangila, Bi. Malima Macha ambaye ni  Katibu, Naibu katibu Bwana James Babu na Mjumbe mmoja Bwana Rashid Mtungi.

JAJI MKUU PROFESA IBRAHIM JUMA AWAASA WANASHERIA KUZINGATIA MISINGI YA TAALUMA


PIC 1
. Jaji Mkuu wa Tanzania Profesa Ibrahim Juma (pili kulia), Waziri wa Katiba na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi (pili kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge (kulia) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Katiba na Sheria Profesa Sifuni Mchome wakiimba wimbo wa taifa kabla ya kuanza mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma unaofanyika Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.
PIC 2
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, akiwahutubia washiriki wa mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma (hawako pichani). Kwenye hotuba yake Profesa Juma amewaasa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma kuzingatia misingi wa maadili kwenye utekelezaji wa majukumu yao.
PIC 3
Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, akitoa neno la utangulizi mbele ya wanasheria waliohudhuria mkutano wa pili wa wanasheria wa walio kwenye utumishi wa umma.
PIC 4
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma (katikati waliokaa) kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria ufunguzi wa mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma. Mkutano huo wa siku mbili unafanyika jiji Dodoma, ukumbi wa mikutano Chuo cha Mipango. 
PIC 5
Wanasheria kutoka Wizara, Serikali za Mitaa, Mashirika, Wakala na Idara  za Serikali wakifuatilia kwa makini hotuba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibarhim Juma, wakati wa ufunguzi wa mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma.
……………………….
Na. Idara ya Habari-MAELEZO
Jaji Mkuu wa Tanzania, Profesa Ibrahim Juma, amewaasa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma kuzingatia misingi ya taaluma wakati wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
Kauli hiyo ameitoa wakati akifungua mkutano wa pili wa wanasheria walio kwenye utumishi wa umma unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Chuo cha Mipango, jijini Dodoma.
“Mkiwa maafisa wa Mahakama tunawatazamia kufanya kazi zenu kwa kuzingatia misingi ya taaluma iliyowekwa kwa kuzingatia maadili, weledi, uwazi na usiri” alisisitiza he Profesa Juma.
Profesa Juma pia amewakumbusha wanasheria hao walio kwenye utumishi wa umma kuhakikisha  kuwa sheria wanazosimamia zinalenga kuleta ustawi wa wananchi wanyonge na kuiwezesha serikali kutimiza azma yake ya kifanya Tanzania iweze kufikia hadhi ya  nchi ya kipato cha kati ifikapo mwaka 2025.
Vilevile, wanasheria hao wa serikali wameaswa kuzingatia matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika kutekeleza majukumu yao ili kuendana na kasi ya mabadiliko ya karne ya 21.
Aliongeza kuwa, wanasheria wanalo jukumu kubwa la kukidhi matarajio ya wananchi ikiwemo Dira ya Taifa ya Maendeleo ya 2025,  amani, usalama, umoja, utawala bora, na kujenga uchumi imara.
Kabla ya Jaji Mkuu Profesa Juma, kuhutubia mkutano huo Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palagamba Kabudi  alimshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli kwa kufanya mabadiliko katika muundo wa Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali ambao unategemewa kuleta ufanisi. Kwenye mabadiliko hayo yaliyoidhinishwa na Rais Magufuli, yamesababisha kuanzishwa kwa Ofisi ya Taifa ya Mashtaka na Wakili Mkuu wa Serikali.
Mkutano huo wa siku mbili unawakutanisha wanasheria zaidi ya mia tisa kutoka Wizara, Serikali za mitaa, Mashirika, Wakala na Idara mbalimbali za Serikali.

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti yaendelea na vikao vyake jijini Dodoma


_T6A2330
Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango akifafanua
jambo mbele ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti iliyokutana leo
Jijini Dodoma iliyokutana leo Jijini Dodoma, kushoto kwake ni
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mheshimiwa George Simbachawene. (Picha na
Ofisi ya Bunge)
_T6A2342
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George
Simbachawene akichangia jambo mbele ya Kamati hiyo iliyokutana leo
Jijini Dodoma, Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa
Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Bunge)
5T6A2282
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Mheshimiwa George
Simbachawene akichangia jambo mbele ya Kamati hiyo iliyokutana leo
Jijini Dodoma, Kulia kwake ni Waziri wa Fedha na Mipango Mheshimiwa
Dkt. Philip Mpango. (Picha na Ofisi ya Bunge)

DK SHEIN ATEMBELEA KITUO CHA UTAFITI MIFUGO LANGONI.


DSC_4382
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kulia) akiangalia mwani katika eneo la Taasisi ya  Utafiti wa Mifugo Zanzibar, Dole Wilaya ya Maghribi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo wakati alipotembelea akiwa katika ziara maalum,[Picha na Ikulu.] 30 Aug 2018.
DSC_4673
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akiuliza suala kwa Katibu Mtendaji wa Kamisheni ya Ardhi Ahmed Abrahmani Rashid (kulia) alipofika kutembelea Eneo la ujenzi wa Hospitali kubwa ya Rufaa inayotarajiwa kujengwa Binguni  Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja  leo akiwa katika ziara maalum,(katikati) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Hassan Khatibu Hassan,[Picha na Ikulu.] 30 Aug 2018. 
DSC_4472
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuuliza suala Mtafiti wa Magonjwa na Uzalishaji Mifugo Dkt.Waridi Abdulla Mussa (kulis) alipokuwa akipata maelezo kutoka kwa Mtafiti huyo alifikas kuasngaslias kuku wa asili (kienyeji) akiwa katika ziara ya kutembelea  katika eneo la Taasisi ya  Utafiti wa Mifugo  Dole Wilaya ya Maghribi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo,[Picha na Ikulu.] 30 Aug 2018. 
DSC_4791 copy
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (wa pili kushoto) akimuuliza suala mtaalam wa Ramani kutoka Wizara ya Ardhi,Maji na Nishati Nd,Juma Ameir (kulia) alipokuwa akiangalia ramani alipotembelea Eneo la ujenzi wa Hospitali kubwa ya Rufaa  inayotarajiwa kujengwa Binguni Katika  Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo  akiwa katika ziara maalum,(kushoto) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Hassan Khatibu Hassan,[Picha na Ikulu.] 30 Aug 2018. 
DSC_4395
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya angalia mwani katika eneo la Taasisi ya  Utafiti wa Mifugo  Dkt.Kassim Gharib (wa pili kulia)  wakati alipotembelea katika eneo la Taasisi hiyo iliyopo   Dole Wilaya ya Maghribi “A” Mkoa wa Mjini Magharibi Unguja leo wakati alipotembelea akiwa katika ziara maalum,[Picha na Ikulu.] 30 Aug 2018.
DSC_4841
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) akifuatana na Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Hassan Khatibu Hassan(kushoto) alipotembelea Eneo la ujenzi wa Hospitali kubwa ya Rufaa  inayotarajiwa kujengwa Binguni Katika  Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja leo (kulia) Mhe.Haji Omar Kheir Kaimu Waziri wa Kilimo,Maliasili,Mifugo na Uvuvi pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,tawala za Mikoa,Serikali za Mitaa na Idare malum za SMZ Mhe.Haji Omar Kheri, [Picha na Ikulu.]

RAIS MAGUFULI MGENI RASMI KWENYE UZINDUZI WA TAMASHA LA URITHI FESTIVAL JIJINI DODOMA

NA. LUSUNGU HELELA-DODOMA
RAIS wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Magufuli, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama Urithi Festival, Celebrating Our Heritage litakalozinduliwa rasmi  kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dodoma,  Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga amesema lengo la Tamasha  hilo  ni kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.

Aidha, Amesema kwa kutambua hazina kubwa ya malikale na utamaduni wa makabila zaidi ya 128 yaliyopo nchini, tamasha hilo litaongeza wigo wa mazao ya utalii kwa kukuza utalii wa utamaduni wa malikale hatua ambayo itaongeza ushindani wa Tanzania kama kituo bora cha utalii kwenye masoko mbalimbali duniani.

Ameongeza kuwa Urithi  Festival itasadia kukuza utalii wa ndani kwa kuongeza muda wa watalii wa kimataifa kukaa nchini kwa vile Tamasha hilo lifanyika katika kipindi ambacho watalii wengi wanatembelea Tanzania.

Naibu Waziri huyo amesema kutokana na watalii kuongeza muda wa kukaa nchini kutaleta faida kwa wananchi na uchumi wa nchi kwa ujumla

Aidha, Naibu Waziri huyo ametaja mikoa  sita pamoja na  tarehe zake  ambayo Tamasha hilo  linafanyika kitaifa wa upande wa  jiji la Dodoma tamasha hilo litafanyika Septemba 15 hadi tarehe 22 na kwa Zanziba litafanyika Septemba 23 hadi 29.

Pia, kwa upande wa  Dar es Salaa na Mwanza tamasha hilo litafanyika Septemba 29 hadi Oktoba 6.
Aidha, kwa upande  wa Wilayani Karatu tamasha hilo litafanyika Oktoba 8 hadi  12, huku Jijini Arusha tamasha hilo linatarajiwa  kutafanyika Oktoba 8 hadi 13 mwaka huu. 

Amesema tamasha hilo kutakuwa na shughuli mbalimbali kama vile sherehe za uzinduzi na kilele, kuenzi lugha adhimu ya Kiswahili na kutoa tuzo kwa wasanii na wadau wa Urithi.

Ameongeza kuwa Tamasha hilo litapambwa na shamrashamra za carnival ya mirindimo ya urithi, burudani za ngoma za asilil, muziki na kwaya pamoja n asana na maonesho ya bidhaa ya wadau.

Katika hatua nyingine, Naibu Waziri huyo amesema kuwa Tamasha hilo litahusisha makongamano ya wataalamu, usiku wa urithi, ziara ya kutembelea vivutio vya utalii pamoja na kunadi urithi katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari kupitia themes za Mvalishe, Misosi ya Kwetu na Michongo ya Urithi.

Tamasha la Urithi Festival litakuwa linafanyika kila mwezi Septemba ya kila mwaka kuanzia mwaka huu.  
1
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya   Urithi Festival walioshiriki kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari uliofanyika leo jijini Dodoma. Tamasha hilo linalotarajiwa kuzinduliwa Septemba 15, 2018 na  kuenzi, kudumisha, kuburudisha na kujifunza masuala muhimu yanayohusu Urithi wa Mtanzania hususani tamaduni zetu, historia, malikale na maliasili.
2

3
 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Japhet Hasunga akizungumza na Waandishi wa Habari leo jijini Dodoma kuwa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli, anatarajia kuwa mgeni rasmi kwenye Tamasha la Mwezi wa Urithi linalotambulika kama ‘’Urithi Festival, Celebrating Our Heritage’’ litakalozinduliwa rasmi  kitaifa katika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma Septemba 15, 2018.
4

Baadhi ya Wajumbe wakiangalia  nembo ya Urithi Festival inakayotumika kwenye Tamasha hilo.

  (Picha zote  na Lusungu Helela-WMU)

RAIS DKT. MAGUFULI AZUNGUMZA NA MADIWANI PAMOJA NA WATUMISHI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA CHATO MKOANI GEITA


1
59Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Madiwani, Viongozi mbalimbali pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato katika mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine katika picha ni Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri Semeon(kushoto) na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Eliud Mwaiteleke(kulia). 
10
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mara baada ya kumaliza mkutano huo na Madiwani, Viongozi mbalimbali pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato. Wengine katika picha ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Christian Manunga wapili kutoka (kulia) mstari wa kwanza mbele, Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri Semeon watatu kutoka (kulia), Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani, wanne kutoka (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Eliud Mwaiteleke.
11
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mara baada ya mkutano huo uliofanyika katika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita. Wengine katika picha mstari wa mbele ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Christian Manunga wakwanza kutoka (kulia) mstari wa kwanza mbele, Mkuu wa Wilaya ya Chato Eng. Mtemi Msafiri Semeon wapili kutoka (kulia), Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani wapili kutoka kushoto pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Chato Eliud Mwaiteleke.
12
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwapungia mkono Madiwani pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato wakatika akiondoka katika Ofisi za Halmashauri hiyo Chato mkoani Geita.
13
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwasili katika ukumbi wa Mikutano wa Halmashauri ya Chato kwa ajili ya mkutano na Madiwani, Viongozi mbalimbali pamoja na Watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato mkoani Geita.
14
Baadhi ya Watumishi wa halmashauri ya Wilaya ya Chato wakifatilia kwa makini wakati Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akizungumza masuala mbalimbali katika ukumbi wa Halmashauri hiyo Chato mkoani Geita. 
PICHA NA IKULU