Wauaji wa wanawake Mto wa Mbu hawa hapa....Polisi yawadaka


Monduli:Jeshi LA Polisi MkoaniArusha limewafikisha mahakamani washukiwa watatu kati ya Tisawaliokamatwa  kuhusiana na mauaji ya wanawake katika kata ya Mto wa Mbu wilaya ya Monduli mkoaniArusha.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ,Ramadhani Ng'anzi amesema watu hao wamefikishwa mahakamanibaada ya jeshi hilo kuendesha msako mkali juu ya matukio ya mauaji ya wanawake yanayotokea  katika kataya MTO wa Mbu ,Majengo na Migungani.

Amewataja watuhumiwa hao kuwa ni Richard Msuya(22),Babuu William(24)na Francis Charles(21)wotewakiwa wakazi wa Kigongoni,Mto wa Mbu,wilaya ya Monduli
Aidha amesema kuwa katika kukabiliana na matukio ya uhalifu jeshi hilo limeanzisha mpango wa ujenzi wa kituo kikubwa cha Polisi kitakachoweza kubeba askari wengi na kuongeza doria katika maeneo yote yenye uhalifu sugu .

Awali takribani tisa wa jinsia ya kike katika kata za Mto wa Mmbu ,majengo na Migungani wilayani humo wameripotiwa kuuawa katika vifo vyenye utata vinavyoshabihiana na miili yapo kukutwa imetelekezwa ,huku  mauaji hayo yakihusishwa na vitendo vya  ubakaji,Ushirikina na uhalifu usio wakawaida.

Moja ya matukio yakusikitisha yaliyotikisa wakazi wa kata ya Mto wa Mmbu ni tukio julai 10,2018 ambapo mwili wa  mwanamke ,Ruth Elias Meena(49) mkazi wa Kigongoni ambaye ni mama wa watoto wawili, ulikutwa katika mtaro wa jeshi akiwa uchi wa mnyama na jeraha kisogoni ukiwa umetelekezwa.

Mzazi mwenzake na marehemu,aitwaye Mathiasi Mtei(61)anasimulia huku akibubujikwa na machozi kwamba siku ya tukio alipata taarifa juu ya kuuawa kwa mama mtoto wake na kusema kuwa anashindwa kulielezea zaidi tukio hilo kwani limemuuma sana mpaka sasa akiangalia picha yake inamwongezea machungu.

Aidha Mtei ambaye alizaa na marehemu mtoto mmoja  aitwaye Vickta Mathias(24)anasema kuwa marehemu aliuawa katika mazingira ya kutatanisha na alishuhudia mwili wa marehemu akiwa na jeraha la damu mbichi kisogoni na shingo ikiwa imevunjwa na kwamba mpaka sasa hafahamu  aliyehusika na  tukio hilo.

Akizungumzia tukio la kuuawa kwa mama yake mzazi,mtoto mkubwa wa marehemu aitwaye,Sarah Meshacky(31)anasema kwamba siku ya tukio mama yake aliondoka nyumbani kwake ,majira ya saa 3 usiku eneo la Kigongoni alidai anaenda kumwona mdogo wake aitwaye Charles Mtei ambaye alimpatia pesa kwa ajili ya kuwasilisha kwenye vikoba,hata hivyo marehemu hakurejea tena hadi kesho yake alipopata taarifa za mamama yake kukutwa ameuawa mtaro wa jeshi.

Naye Diwani wa kata ya Mto wa Mbu,Sarah Lukumay ameeleza kusikitishwa na matukio ya kuuawa kwa wanawake likiwemo la marehemu,Ruth ambapo anabainisha kwamba takribani wanawake tisa wameuawa huku sababu za vifo hivyo ikiwa haijulikani.

Ameeleza kushuhudia baadhi ya matukio ya kikatili na kinyama yanayotokea kwa wanawake likiwemo tukio la kuuawa kwa marehemu,Shikensia Boaz ambaye aliuawa wakati akitoka Sokoni .

Pia amemtaja marehemu  Vicky Kivuyo ambaye mwili wake ulikutwa katika mto Mahamudu kwenye shamba la migomba akiwa amebakwa na kuingiziwa chupa sehemu za siri huku mwili huo ukiwa na majereha mbalimbali.

Amesema katika kata ya Majengo msichana aliyefahamika kwa jina moja la Ndamaa alikutwa amekufa darajani kwenye shamba la Mahamudu.

Katika tukio jingine mama wa kimasai (jina halikufahamika mara moja)mwili wake ulikutwa umeharibika vibaya katika shamba la jeshi na sehemu za siri kulikutwa vipande vya miti.

Hata hivyo alishindwa kufafanua iwapo matukio hayo yanahusiana na masuala ya ushirikina  ama ni uhalifu wa kawaida.Ameliomba jeshi la polisi kuongeza nguvu katika uchunguzi wake waweze kuwatia mbaroni wahusika kwani hadi sasa wananchi wanalazimika kulala saa 12 jioni kuogopa kuuawa.

Baadhi ya wakazi wa kata ya Mto wa Mmbu,Emanuel Kiula Tabitha George wamedai kuingiwa na hofu kubwa juu usalama wa maisha yao hasa  wanawake kwani kwa sasa wam,elazimika kutotoka nyumbani ifikapo saa 12 jioni wakihofia maisha yao jambo ambalo linawafanya waishi kama wakambizi ndani ya nchi yao .
Wamelitaka jeshi la poliisi mkoani hapa kukomesha uhalifu huo kwani hasi sasa wanashangaa kutokamatwa kwa wahusika huku matukio hayo yakiendelea kushamiri.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni