ZIARA YA WAZIRI WA MADINI ANGELA KAIRUKI KWENYE MIGODI YA MADINI YA RUBY LONGIDO


Waziri wa Madini Angela Kairuki amewataka wachimbaji wa madini ya Vito ya Rubi kutanguliza uzalendo kwa taifa lao na kuacha kushiriki vitendo vya utoroshaji wa madini hayo kupitia mpaka uliopo jirani na wilaya ya Longido.
????????????????????????????????????
Mkuu wa wilaya ya Londigo Frank Mwaisumbe akiuelekeza msadara wa Waziri wa Madini Angela Kairuki aliyefanya ziara kwenye mgodi wa Mundarara Ruby Miningi unaomilikiwa na mwekezaji Rahim Mollel uliopo Kata ya Mundarara katika ziara hiyo aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo. 
????????????????????????????????????
Waziri wa Madini Angela Kairuki akiangalia kwa makini mgodi wa madini ya Ruby wa Mundarara unaomilikiwa na mwekezaji Rahimu Mollel ambapo alifanya ziara hiyo kujionea shughuli za uchimbaji na kufahamu changamoto zinazowakabili.
????????????????????????????????????
Mwekezaji wa mgodi wa Mundarara Ruby Mining uliopo Longodi mkoani Arusha Rahim Mollel akiongoza msafara wa Waziri wa Madini Angela Kairuki aliyefuatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kutembelea mgodi huo. 
????????????????????????????????????
Mwekezaji wa mgodi wa Mundarara Ruby Mining uliopo Longodi mkoani Arusha Rahim Mollel akimuonyesha Waziri wa Madini kipande cha Ruby mara baada ya kuvunja jiwe gumu. 
????????????????????????????????????
Waziri wa Madini Angela Kairuki akisoma Leseni ya uchimbaji ya kampuni ya Sendeu inayomilikiwa na aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha na Mbunge wa zamani Longido Michael Laizer 
????????????????????????????????????
Waziri wa Madini Angela Kairuki akiangalia mazingira ya mgodi  wa uchimbaji madini ya vito ya Ruby  unaomilikiwa na Kampuni ya Sendeu iliuopo chini ya aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha na Mbunge wa zamani Longido Michael Laizer.
????????????????????????????????????
Waziri wa Madini Angela Kairuki akicheza ngoma za kabila la Wamaasai kabla ya kuwahutubia wananchi na wakazi wa Kijiji cha Mundarara yalipo machimbo ya madini ya vito ya Ruby wilayani Longido mkoani Arusha. 
????????????????????????????????????
Waziri wa Madini Angela Kairuki akihutubia wananchi na wachimbaji wadogo wa madini ya vito ya Ruby katika eneo la Kijiji cha Mundarara wilayani Longido mkoani Arusha 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni