VICTOR MASANGU, CHALINZE
MKUU mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa amewataka vijana ambao wanahitimu mafunzo ya jeshi la akiba kuhakikisha wanakuwa wazalendo na nchi yao na kuachana kabisa na vitendo vya kujiingiza katika matukio ya kihalifu na badala yake wahakikishe wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa kwa lengo la kuweza kulinda hali ya ulinzi na usalama wa wananchi na mali zao.
Kauli hiyo aliitoa wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo ya awali ya jeshi la akiba ambayo yamefanyika katika kata ya Bwilingu na kuwajumusiha vipana wapatao 183 kutoka katika halmashauri ya Chalinze Wilayani Bagamoyo Mkoa wa Pwani.
Mkuu huyo pia aliwahimiza vijana hao kuhakikisha wanakuwa na nidhamu ya hali ya juu katika kipindi chote cha mafunzo hayo ya kijeshi na kuzingatia maelekezo ambayo wanapatiwa na walimu wao kwa lengo la kuweza kujifunza mbinu mbali mbali ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa katika kulilinda Taifa la Tanzania na kuweza kukabiliana na wimbi la matukio ya uhalifu.
“Napenda kuchukua fursa hii kuwapongeza vijana ambao mmeweza kujitokeza katika mafunzo haya ya jeshi la akiba,lakini kitu kikukbwa ninawaomba muwe wazalendo na nchi yenu kwa kuhakikisha mnazingatia sheria na taratibu za nchi ikiwa ni sambamba na kuyatumia vizuri mafunzo mliyopatiwa kwa maslahi ya nchi na sio vinginevyo,”alisema
Kwa upande wake Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku alibainisha kuwa mafunzo hayo yatakuwa ya miezi minne na nusu ambapo vijana hao wataweza kujifunza mbinu mbali mbali za kivita ambazo zitaweza kuwa ni mkombozi mkubwa kwa maslahi ya Taifa.
“Katika mafunzo haya vijana ambao walijitokeza hapo awali walikuwa ni 211 lakini baadhi yao wameshindwa kuendelea kutokana na sababu mbali mbali hivyo ambao wanaendelea kwa sasa na ni vijana wapatao 183 ambao wametokea katika kata ya bwilingu, ambapo wataweza kupata mafunzo mbali mbali ya kijenzi kwa kipindi cha muda wa wiki 18 alisema Chinguku”
Naye Diwani wa kata ya Bwilingu Lucas Lufundo alisema kwamba mafunzo hayo yataweza kuwasaidia vijana kwa kiasi kikubwa kudumisha hali ya ulinzi na usalama katika maeneo mbali mbali na kwamba kutaweza kupunguza wimbi la vijana wengi ambao walikuwa wanakaa vijiweni bila ya kujishughulisha na kazi pamoja na kupunguza na changamoto ya wimbi la uhalifu.
VIJANA hao wapatao 183 kutoka halmashauri ya Chalinze katika mafunzo hato ya wiki 18 wataweza kupta fursa ya kujifunza masomo mabli mbali ya kivita na yale ya kawaida ikiwemo ujanja wa porini,usomaji wa ramani, huduma ya kwanza usalama wa raia,utimamu wa mwili, uhamiaji,pamoja na vitendo katika medani pamona na kujifunza mapambano dhidi ya rushwa.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani kutoka kata ya Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Kawawa wa kati kati akirukaruka mara baada ya kufungua mafunzo rasmi ya jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 hawapo pichani kutoka kata ya Bwilingu katika halmashauri ya Chalinze pembeni yake kulia ni Mshauri wa jeshi la akiba Wilayani Bagamoyo Maj Chinguku.
Mkuu mpya wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Rashid Kawawa kulia akiwa na Mshauri wa jeshi la akiba wilayani humo wa kushoto Maj Chinguku wakati wa sherehe za ufunguzi rasmi wa mafunzo wa jeshi la akiba kwa vijana wapatao 183 ambayo yamefanyika katika kata ya Bwilingu halmashauri ya Chalinze.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni