Mkurugenzi wa fedha na mpango katika hospitali ya Rufaa Bugando, mtawa Suzan Bathlomeo amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka gorofani muda mfupi baada ya kutoka kusali misa ya saa 12:00 asubuhi, leo Jumanne Agosti 28, 2018.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jonathan Shana
amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa taarifa kamili
atazungumza na waandishi wa habari baadaye.
Kwamjibu wa ofisa uhusiano wa Bugando, Lucy Mogele amesema
mtawa huyo amefariki dunia leo alfajiri, huku akibainisha kuwa hospitali
hiyo haina mamlaka ya kuzungumziwa suala hilo na kutaka litafutwe
shirika la watawa la Kagera, ambalo makao makuu yake yapo mjini Bukoba
mkoani Kagera.
“Ni kweli Sister Suzan amefariki dunia baada ya kujirusha
kutoka ghorofani lakini Bugando hatuna mamlaka ya kuzungumzia suala
hilo,” amesema Lucy.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni