Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst)
Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akimtunuku cheti Katibu Mkuu wa Wizara ya
Fedha na Mipango, Bw. Doto James baada ya kuhitimu kozi fupi ya tano ya
Viongozi iliyofanyika katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi,
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya
Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Kapt. (Mst)
Mhe. George H. Mkuchika (Mb) akipokea zawadi ya tai, kutoka kwa Mkuu wa
Chuo cha Taifa cha Ulinzi (NDC) Luteni Jenerali, Paul Massao, baada ya kufungua
kozi fupi ya tano ya Viongozi, iliyofanyika katika Chuo cha Taifa
cha Ulinzi, jijini Dar es Salaam.
JAMHURI YA
MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA RAIS
|
Simu Na: +255 (026) 2963630 Menejimenti ya Utumishi wa
Umma Nukushi: +255 (026) 2963629
na Utawala Bora, Barua Pepe: ps@utumishi.go.tz Jengo la
Taaluma Na. 1,
Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM),
18
Barabara ya Mkalama,
S.L.P. 670,
40404 DODOMA.
TAARIFA KWA UMMA
VIONGOZI NA WATUMISHI NCHINI
WAKUMBUSHWA KUTEKELZA MAJUKUMU YAO KWA KUTANGULIZA MBELE MOYO WA UZALENDO NA MASILAHI
YA TAIFA
Viongozi
na Watumishi nchini wamekumbushwa kutanguliza mbele moyo wa uzalendo na
masilahi mapana ya taifa wanapotekeleza majukumu yao ili kupeleka maendeleo ya
taifa mbele na kuimarisha usalama wa taifa.
Hayo
yamesemwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na
Utawala Bora, Kapt (Mst)
Mhe. George H. Mkuchika (Mb) wakati akifunga kozi fupi ya tano kwa viongozi
iliyofanyika Chuo cha cha Taifa cha Ulinzi - Tanzania (NDC) jijini Dar es
Salaam.
Mhe.
Mkuchika amesema, ni matumaini kuwa washiriki waliohudhuria kozi hiyo, utendaji
wao wa kazi utabadilika kwa kuwa na tija kwani sasa mbinu zote zinazohusu namna
ya kufikiri kimkakati, kufanya tathmini katika mambo mbalimbali ili kufikia
maamuzi wamezipata.
“Sasa
mnatambua dhana ya usalama wa Taifa vema na kwa mapana zaidi, si kulinda mipaka
na mali za wanajamii tu, bali pia inahusisha kutunza mazingira, kuwa na chakula
cha kutosha, kupiga vita rushwa na madawa ya kulevya na mengine mengi ambayo ninyi
mnayafahamu zaidi,” Mhe. Mkuchika amesema na kuongeza kuwa usalama wa watu ni
muhimu kuliko jambo jingine lolote, hivyo masuala ya usalama yawe ni sehemu ya
kuzingatia katika utendaji wa kila siku na hasa pale maamuzi yanayogusa masilahi
ya nchi na jamii yanapotolewa.
Aidha,
Mhe. Mkuchika amesema, Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kwa
dhati kuipeleka nchi katika Uchumi wa Viwanda, lakini suala la rushwa limekuwa
kikwazo kikubwa kufikia lengo hilo, hivyo ni jukumu la viongozi wote kutoa
majawabu ya namna gani malengo yatafikiwa.
Kwa
upande wake, Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi -Tanzania, Luteni Jenerali Paul
Massao ameishukuru Serikali kwa kuhakikisha viongozi na watumishi wengine wanahudhuria
kozi hiyo muhimu kwa masilahi ya taifa.
Jumla
ya wahitimu 24 walikabidhiwa vyeti, baadhi yao wakiwa ni Waheshimiwa Naibu
Mawaziri, Makatibu Wakuu, Waheshimiwa Wakuu wa Mikoa, Viongozi wa vyombo vya
Ulinzi na Usalama, Viongozi Waandamizi wa Taasisi za Serikali.
Mtaala
wa kozi hiyo ulilenga katika masuala yanayohusu masilahi, uzalendo na dhana
nzima ya usalama wa taifa.
IMETOLEWA
NA:
KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI
OFISI YA RAIS (UTUMISHI)
TAREHE
18 AGOSTI, 2018
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni