NAIBU WAZIRI KWANDIKWA AIPONGEZA TANROADS MANYARA


IMG-20180802-WA0069
Naibu Waziri wa Ujenzi, Elias Kwandikwa (katikati) akizungumza na wafanyakazi wa Tanroads na Temesa mjini Babati Mkoani Manyara, kulia ni Meneja wa Tanroads Mkoani Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa na Meneja wa Temesa Mkoani Manyara Edwin Ndomba.
IMG-20180801-WA0104
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa akipokewa na Meneja wa Tanroads Mkoani Manyara mhandisi Bashiri Rwesingisa (kulia) alipofanya ziara ya siku mbili Wilaya za Babati, Mbulu na Hanang’ Mkoani Manyara.
Naibu Waziri wa Ujenzi Elias Kwandikwa amewapongeza Tanroads Mkoani Manyara kwa namna wanavyotekeleza wajibu wao kwa kutekeleza ipasavyo miradi ya barabara.
Kwandikwa alisema mara nyingi anafuatilia utendaji kazi wa wafanyakazi wa Tanroads na wamekuwa wanatekeleza miradi ipasavyo ikiwemo ujenzi wa barabara ya Babati-Kondoa.
“Pamoja na utendaji kazi wenu mzuri nitawaachia mawasiliano yangu ili mtu akiwa na jambo lolote tuweze kuwasiliana,” alisema Kwandikwa.
Meneja wa Tanroads Mkoani Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa alisema alimshukuru Naibu Waziri huyo kwa pongezi hizo na akamuhakikishia kuwa hawatabweteka.
“Tutaendelea kuchapa kazi na tunashukuru kwa kutambua utendaji kazi wetu nasi hatutakuangusha tutasomba mbele,” alisema mhandisi Rwesingisa.
Hata hivyo, mmoja kati ya katibu muhtasi wa Tanroads Mkoani Manyara, Ziada Yasini alitoa ombi kwa ajili ya kupatiwa ajira ya kudumu.
Dereva wa Temesa Benjamin Nguki aliomba kupatiwa mafunzo mara kwa mara ili kuendana na teknolojia mpya ya kisasa inayotoka mara kwa mara.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni