Naibu waziri Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe,Lucas Boniphace Magembe wakiwa katika boti ya kizamani, tayari kwa ajili ya safari ya kwenda katika kisiwa cha Gana
katika ziara yake ya kanda ya ziwa ya kuwahamasisha wavuvi ufungaji wa samaki kwa vizimba katika ziwa Victoria.
(picha na Emmanuel Massaka Globu ya jamii)
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kisiwa cha Gana wilaya ya Ukerewe mkoa wa Mwanza ambapo aliwasisitiza polisi pamoja na mgambo wanapoenda kwenye operesheni ya kupambana na uvuvi haramu wawewanaenda na maafisa uvuvi kwa kuwa wao wanajua zana haramu pamoja samaki wasioruhusiwa kisheria.
Naibi Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akipanda boti ya kizamani, tayari kwa ajili ya safari ya kuelekea katika kisiwa cha Gana Wilaya ya Ukerewe kwaajili ya kuhamasisha ufungaji wa samaki kwa vizimba katika Vctoria.
Wananchi wa kisiwa cha Gana wilaya ya Ukerewe wakimsikiliza Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega wapili (kushoto) akiwa ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Sengerema,Lucas Magembe (kushoto) wakiwasili katika kisiwa cha Gana.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni