Jaji aliyewahukumu kifo kesi ya Bilionea Msuya atishiwa Kifo...Ni Salma Maghimbi


Jaji Salma Maghimbi aliyesikiliza kesi ya mauaji ya bilionea Erasto Msuya na kuwahukumu adhabu ya kifo washitakiwa watano, ametishiwa kuuawa na mtu asiyejulikana
Inadaiwa mtu huyo alipiga simu kupitia simu ya mezani(ofisini) na kumtisha kummiminia risasi kama za bilionea Msuya kwa kitendo cha kumhukumu ndugu yake kunyongwa
Mtu huyo alimwambia Jaji kuwa iwapo watashindwa kumuua nyumbani au barabarani, basi wangetekeleza mauaji hayo akiwa katika eneo la mahakama Kuu
Kutokana na vitisho hivyo, Jeshi la Polisi limemuongezea ulinzi Jaji huyo ambaye sasa amehamishiwa divisheni ya Ardhi jijini Dar lakini bado anamalizia kesi zake jijini humo
Msuya aliuawa kwa kupigwa risasi na bunduki ya kivita aina ya SMG Agosti 7, 2013 eneo la Mijohoroni wilayani Hai mkoani Kilimanjaro

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni