MBUNGE wa Mtwara Vijijini (CCM)
ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Bajeti, Hawa Ghasia na
Makamu Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jitu Soni wamejiuzulu nafasi hizo, leo
Jumanne Agosti 28, 2018.
Ghasia na Soni ambaye pia ni
Mbunge wa Babati Vijijini wametangaza uamuzi wao leo asubuhi mbele ya
wajumbe wa kamati hiyo jijini Dodoma.
Bado haijafahamika sababu za viongozi hao kufanya uamuzi ho wa kujiuzulu.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni