TAASISI YA MAENDELEO JIMBO LA VUNJO (VDF) YASEMA GHARAMA UKARABATI WA BARABARA NDANI YA JIMBO HILO HUENDA ZIKAONGEZEKA ZAIDI


Katibu wa Taasisi ya Maeneleo ya Jimbo la Vunjo,James Mbatia akitoa salamu kwa baadhi ya wananchi walioshiriki katika ukarabati wa miundo mbinu ya barabara unaoendelea katika jimbo hilo kwa kuchangia nguvu kazi.
Mmoja wa wananchi waliojitokeza katika ukataji wa miti kupisha upanuzi wa barabara akiandaa mbao kwa ajili ya shughuli nyingine za uakarabati wa barabara hizo. 
Greda likiendelea na kazi ya uondoshaji wa baadhi ya miti iliyokuwa kando ya barabara zinazopanuliwa katika jimbo la Vunjo.
Mafundi kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) wakiondosha Nyaya ili kupisha upanuzi wa barabara hizo.
Shughuli ya upanuzi wa barabara ikiendelea.
Baadhi ya wananchi wakichangia nguvu kazi katika ukarabati wa barabara hizo.
Upanuzi wa barabara mbalimbali ukiendelea katika jimbo la Vunjo. 
Moja ya eneo ambalo kazi ya upasuaji wamiamba ililazimika kufanyika ili kupanua barabara .
Muonekano wa barabara katika maeneo mbalimbali wakati ukaraba huo ukiendelea .
 

Na
Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii,Kanda ya Kaskazini.

TAASISI
ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo(VDF) imesema gharama zilizotengwa awali kwa
ajili ya ukarabati wa Km 272.8 za barabara katika vijiji vyote vya jimbo hilo huenda
zikaongezeka kutokana na kuwepo kwa miamba katika maeneo ambayo yanahitaji
upanuzi.
 Katibu
wa taasisi hiyo,James Mbatia amesema ikiwa imengia wiki ya tatu tangu kuanza
kwa ukarabati kwa baadhi ya maeneo katika barabara hizo tayari wamekutana na
changamoto ya uwepo wa miamba ambayo imelazimika kuvunjwa kwanza .
 “Tulipanga
hii kazi kutumia miezi sita kuimaliza lakini sasa inaweza kuchukua hadi mwaka
mmoja kutokana na changamoto ambazo zimeanza kujitokeza hizi za kukutana na
miamba na wakati mwingine hali ya hewa”alisema Mbatia.
 Mbatia
ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Vunjo alisema awali walipanga kutumia kiasi
cha Sh Bil 7.29 kukamilisha kazi hizo lakini kwa namna shughuli inavyoendelea huenda
gharama ikazidi huku akiendelea kutoa wito kwa wadau kuendelea kuchangia
 “Hadi
sasa tunashukuru kazi inaendelea vizuri tukishirikiana nawenzetu wa
TARURA,TANESCO na tasisi nyingine ,lakini kipekee niombe serikali ione umuhimu
wa kusaidia katika kutatua changamoto hii ya barabara kwa wakazi hawa wa jimbo
la Vunjo”alisema Mbatia.
 Kutokana
na kuendelea kwa shughuli ya ukarabati wa barabara hizo tayari wananchi katika
vijiji vya Shira na Mshiri vilivyopo katika jimbo la Vunjo wameanza kunufaika
na mradi huo unaotekelezwa na Taasisi ya Maendeleo ya jimbo la Vunjo (VDF).
 Shughuli
ya upanuzi wa barabara katika kijiji cha Mshiri,Marangu ikiendelea kwa uondoaji
wa miti iliyo kando ya barabara ya awali sambamba na uondohaji wa Miundo mbinu
ya umeme ili kupisha shughuli za upanuzi.
 Manyara leo
Blog  imefika katika maeneo mbalimbali ya
vijiji vilivyoko katika jimbo la Vunjo na kujionea mitambo ikiendelea na
shughuli za upanuzi wa barabara pamoja na uondoaji wa miti na mawe makubwa
yaliyokuwa katika maeneo ya barabara hizo.
 Happy
Makyao na Neema Temu ni wakazi wa Marangu ambao wanajishughulisha na biashara
ya matunda katika eneo la Marangu Mtoni wakazungumzia adha walizokumbana nazo
kabla ya kuanza kwa ukarabati huo na matumaini yao mara baada ya kukamilika kwa
mrad huo.
 “Kabla
ya matengenezo ya hizi barabara tulikuwa tikipata shida sana kutokana na baadhi
ya maeneo kuwa na vichaka vikubwa na wakati mwingie ilikuwa ni hatari kwa
wanafunzi na wakati mwingine walibakwa kwa sasa tumeanza kuona unafuu mkubwa”alisema
Happy Makyao.
 Kwa upande
wake Neema Tema aliipongeza taasisi ya VDF kwa kazi kubwa waliyoianza katika
jimbo la Vunjo na kwamba kwa sasa maeneo ambay yalikuwa hayafikiki kwa urahisi
na kwa gharama ya juu sasa yanafikika.
 “Kwa
mfano bidhaa zetu tukizisafirisha kutoka maeneo ya juu kuja hapa Marangu Mtoni
,tulikuwa tunatumia kiasi cha Sh 2000 hadi 3000 kwa kutumia pikipiki lakini kwa
sasa baada ya kufanyika ukarabati tunalipa sh 1000.”alisema Temu.
 Exaud
Mamuya Diwani wa kata ya Mshiri,Marangu akaeleza juu ya fursa kwa wananch hao
zinaoztokana na ukarabati wa miundo mbinu ya barabara katika maeneo yao kwa
kukusanya mawe yaliyochimbuliwa na kisha kuyauza.
 “Matengenezo
haya ya barabara yametoa Fursa pia kwa wananchi wanaoishi kando ya barabara
hizo,mfano kupata kibali cha kukata mti wako ilikuwa lazima uingie gharama
,lakini kwa sasa wananchi wanaweza kukata miti yao kwenye maeneo ambayo
barabara zinapanuliwa”alisema Mamuya.
 “Eneo
jingine ambalo wananchi wananufaika nalo ni wakati wa upanuzi wabarabara kuna
Mawe ambayo yamekuwa yakiondolewa barabarni ,wananchi wamekuwa wakiyakusanya na
kuyauza ambapo wamekuwa wakipata hadi sh 80000 kwa lori moja”aliongeza Mamuya.
 Kuanzishwa
kwa Taasisi ya Maendeleo ya Jimbo la Vunjo (VDF) kutasaidia utatuzi wa kero
katika Sekta ya Miundombinu ya barabara ,Elimu ,Afya na Maji ambapo kwa upande
wa miundo mbinu ya barabara,Km 272.8 za vijiji vyote katika jimbo hilo
zinataraji kupitiwa.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni