WAJASIRIMALI WATAKIWA KUJENGA MAZOEA YA KUBADILISHANA UZOEFU


index
Na Ahmed Mahmoud Arusha
Wajasiriamali nchini wametakiwa kujenga mazoea ya kubadilisha uzoefu na Teknolojia ili kuweza kufikia malengo ya uchumi wa kati wa viwanda hapa nchini itakayowasidia kukuza kuinua uzalishaji.
Kauli hiyo imetolewa na katibu Tawala wa mkoa wa Arusha Richard Kwitega wakati akifungua semina iliyoandaliwa na shirika la viwanda vidogo vidogo nchini Sido kwa kushirikiana na shirika la maendeleo la Japan (Jica) ambao wameleta teknolojia mpya ya Kaizen.
Amesema kuwa ili kufikia maendeleo ya uzalishaji wenye tija katika viwanda vidogo vidogo na vikubwa hapa nchini teknolojia hii ya kaizen itasaidia sana viwanda vyetu kuzalisha kwa tija na uchumi kukuwa.
“Wajasiriamali naombeni muwe mnabadilishana uzoefu na kujenga ushirikiano utakaosaidia sekta ya viwanda hapa nchni kukuwa na kuongeza uzalishaji wenye tija usiopoteza bidhaa mnazozalisha”alisema Kwitega
Kwa Upande wake Meneja wa Sido mkoani Hapa Nina Nchimbi alisema kuwa wamepata mkombozi baada ya wenzao shirika la maendeleo la Japan kuja na Teknolojia mpya ya viwanda vidogo ijulikanayo Kaizen itakayosaidia sekta ya viwanda kupiga Hatua kubwa.
Amesema kuwa wamejipanga kwenda na falsafa ya uchumi wa viwanda hivyo teknolojia hiyo imekuja wakati muafaka kwa wajasiriamali hapa nchini kuiochangamkia na ushirikiano wao na japani ni moja ya kujenga uzoefu katika kufikia maengo tarajiwa.
Amesma kuwa huduma ya uendelezaji wa Teknolojia ndio msingi wa kukuza sekta ya wajasiriamali ambayo ndio itasaidia kukuwa kiuchumi na kufikia adhma ya serikali ya viwanda na kufikia uchumi wa kati kwa uzalishaji wenye tija kwa kutumia Kaizen katika viwanda vyetu.
Nae Mtaalamu wa Kaizen kutoka Jica Takao Kikuchi alisema kuwa Tanzania na japan hazina tofauti kubwa katika suala zima la wajasiriamali na viwanda vidogo ndio maana tumekuja hapa kufanya ushirikiano utakaosaidia nchi yenu kufikia katika maendeleo ya sekta hiyo.
Amesema kuwa uzoefu waliofikia Japan katika skta ya viwanda ndio maana wakaja na Teknolojia ya Kaizen ambayo ni mkombozi wa viwanda katika kufikia maelengo ya uzalishaji na suluhu ya changemoto za viwanda vidogo na wajasiriamali kufikia malengo.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni