JESHI LA ZIMAMOTO HUFIKA KWENYE MATUKIO KWA WAKATI LICHA YA KUKABILIWA NA CHANGAMOTO MBALIMBALI

Kuchelewa kufika kwenye tukio husababishwa na mambo yafuatayo:-

(i) Wananchi hususani wanaokuwepo eneo la tukio kuchelewa kutoa taarifa kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kutokana na kuanza kwanza kuokoa mali zilizomo ndani ya Jengo linaloungua bila kutoa taarifa kwanza kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.

(ii) Msongamano wa Magari barabarani, pia madereva kutopisha magari ya Zimamoto yanapokuwa yanakwenda kwenye tukio.

(iii) Umbali kutoka vituo vya Zimamoto hadi maeneo ya pembezoni mwa Miji.

(iv) Ujenzi holela nauwekwaji wa vikwazo kama vile matairi chakavu, vyuma na mawe makubwa kando ya mitaa finyu ya maeneo hayo.

(v) Kutoku wepo kwa majina ya mitaa katika maeneo mapya yaliyopimwa na yasiyopimwa.

Mbali ya changamoto zote hizo Jeshi la Zimamoto na Uokoaji limekuwalikiitikia na kutoa magari ndani ya dakika mbili tokea wito ulipo pokelewa.

WITO KWA WANANCHI:- JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LINATOA WITO KWA WANANCHI KUTOA TAARIFA MAPEMA PINDI WANAPOPATWA NA MAJANGA KAMA VILE MOTO, MAFURIKO, AJARI ZA BARABARANI NA MAJANGA MENGINEYO KWA KUPIGA SIMU YA DHARURA 114 KABLA TUKIO HALIJALETA MADHARA MAKUBWA.

MAJALIWA ASHIRKIKI MKUTANO WA APRM- NAIROBI

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akiwa katika maungumzo na Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya (kulia), Rais wa Msumbiji, Filipe Nyusi (wapili kulia) na Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU), Madame Nkosazana Dlamini- Zuma kabla ya kuanza kwa Mkutano wa African Peer Review Mechanism Forum (APRM) kwenye ukumbi wa hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi Agosti 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kabla ya kuanza kwa Mkutano wa African Peer Review Mechanism Forum (APRM)kwenye ukumbi wa hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi Agosti 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na ujumbe wake wakishiriki katika Mkutano wa African Peer Review Mechanism Forum (APRM)kwenye ukumbi wa hoteli ya Intercontinental jijini Nairobi Agosti 26, 2016. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

MBUNGE WA ARUSHA MJINI MBARONI KWA UCHOCHEZI

Image result for mbunge arusha mjini picha 

Na Mahmoud Ahmad Arusha
JESHI la polisi mkoa wa Arusha linamshikilia mbunge wa jimbo la Arusha Mjini  Godbless Lema (CHADEMA) kwa tuhuma za kutoa na  kusambaza maneno ya uchochezi katika mitamndao mbalimbali ya kijamii.
 
Akithibitisha kukamatwa kwa mbunge  Lema mbele ya vyombo vya habari kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Charles Mkumbo alisema Lema alikamatwa jana majira ya saa 12;00 asubuhi nyumbani kwake Njiro akiwa amelala.
Alisema baadhi ya menono hayo ni “Kama mauti imepoteza utukufu wake hakuna statement ya kurudisha nyumba Arusha kuandamana”
 
Kwa mujibu wa kamanda maneno hayo aliyotoa Lema ni ya uchochezi na kuvuruga amani ya nchi na ndiyo maana wanamshikilia kwa ajili ya mahojiano juu ya kaluli zake hizo
.
Alisema watanzania wanatambua umuhimu wa amani na hakuna mtu aliyejuu ya sheria hivyo ni vyema tukaheshimu amani na utulivu tulionao.
Aidha alisema utii wa sheria bila shurti ni vyema ukazingatiwa ili kuepuka machafuko ambayo yanaweza kutokea kutokana na maneno hayo ya uchochezi.
Hata hivyo polisi baada ya kumkamata  wameifanyia upekuzi nyumba yake ili kubaini iwapo kuna vitu vyenye kuashiria uchochezi zikiwemo fulana ama bendera zenye maandishi ya  Ukuta.

CCM YAPIGA MARUFUKU MAKUNDI NDANI YA CHAMA HICHO

Mkutano wa kwanza wa TEHAMA ambao umeandaliwa na Tume mpya ya Teknolojia Habari na Mawasiliano Wanfanyika dar

 -   Afisa wa TTCL, Diana Obed  akitoa maelezo ya bidhaa ya TTCL 4G  kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura   na Mkurugenzi wa Mawasiliano kutoka katika Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Clarence Ichwekeleza katika Mkutano wa kwanza wa TEHAMA ambao umeandaliwa na Tume mpya ya Teknolojia Habari na Mawasiliano uliofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es salaam.
 Mshiriki wa  Mkutano wa TEHAMA akipata maelezo ya huduma ya 4G LTE kutoka kwa Afisa wa TTCL
Washiriki wa  Mkutano wa TEHAMA wakipata maelezo ya huduma ya 4G LTE kutoka kwa  Afisa wa TTCL
 Washiriki wa  Mkutano wa TEHAMA wakipata maelezo ya huduma ya TEHAMA na mawasiliano ya simu zitolewazo na kampuni kutoka kwa Maafisa wa TTCL.
Mshiriki wa  Mkutano wa TEHAMA akipata maelezo ya huduma za TTCL
    
 Washiriki wa mkutano wakinunua laini za 4G  LTE katika mkutano huo
 
Washiriki wakipata maelezo ya TTCL 
 Washiriki wa mkutano wakinunua laini za 4G  LTE katika mkutano wa TEHAMA,
 
 Washiriki wa mkutano wakinunua laini za 4G  LTE katika mkutano huo.

Afisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dr Kamugisha Kazaura akizungumza na mshiriki wa mkutano wa TEHAMA, uliofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere 

PSPF YAKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO KWA JESHI LA MAGEREZA UKONGA JIJINI DAR ES SALAAM


 
 
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Abdul Njaidi, (kushoto), akimkabidhi seemu ya vifaa vya michezo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, Agosti 25, 2016. Vifaa hovyo ni vya michezo ya ngumi, mpira wa miguu na mpira wa pete. 
 

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, umekabidhi vifaa vya michezo kwa wanamichezo wa Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam na kasha kufuatiwa na PSPF bonanza la michezo ya mpira wa miguu, mpira wa pete, Ngumi na Judo. 


Akikabidhi vifaa hivyo vya michezo Agosti 25, 2016, Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo, Abdul Njaidi, alisema, PSPF imeamua kutoa vifaa hivyo ili kuunga mkono juhudi za serikali katika kuinua michezo nchini. 

“Nyinyi mkiwa kama sehemu kubwa ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, tunayo furaha kutoa vifaa hivi vya michezo kwani baada ya kutekeleza majukumu mazito ya kitaifa mnahitaji kushiriki michezo ili kujenga afya lakini pia kuinua vipaji vyenu,” alisema na kuongeza, 

“Nichukue fursa hii kuwahamasisha mjiunge na PSPF kwani kuna faida nyingi mtapata kutokana na kutoa mafao mbalimbali yatakayoboresha maisha yenu kama ambavyo kauli mbiu yetu inavyosema, PSPF ni chaguo lako sahihi na kamwe hutajutia uamuzi wako wa kujiunga na Mfuko huu.” Alisisitiza Njaidi. 


Akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya wanamichezo hao, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza-Ukonga, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, aliishukuru PSPF kwa msaada huo wa vifaa vya michezo kwani vitawawezesha wanamichezo hao kushiriki michezo katika mazingira bora ya kiuanamichezo. 

Baada ya makabidhiano hayo, wanamichezo hao walionyesha uwezo wao katika michezo ya mpira wa miguu, ngumi, mpira wa pete, na judo. 
Afisa Masoko wa PSPF, Magira Werema, (kushoto), akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo, Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari. NA K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
Afisa Matekelezo (Compliance), wa PSPF, George Mnasizu, (kushoto), akigawa vipeperushi vyenye maelezo ya kina ya huduma zitolewazo na Mfuko huo kwa baadhi ya wanamichezo wa Jeshi la Magereza.
Njaidi akiwa na Mkuu wa Kikosi hicho, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Kikosi Maalum cha Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Rajabu Nyange Bakari, na wacheza judo wa kikosi hicho wakiwa katika picha ya pamoja na vipeperushi vya PSPF.
Njaidi akimkabidhi sehemu ya vifaa hicho, Nahodha wa timu ya mpira wa pete (Netball), wa timu ya Magereza Ukonga, Pili Enzi.
Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo kocha wa soka wa timu ya Magereza, Sajenti Hassan Mulego.
Njaidi akikagua timu ya soka ya Magereza Ukonga, ambayo ilimenyana na Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, wakati wa bonanza hilo la michezo.
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza.
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza.
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza.
Hizi ndio Gloves na flana zilizotolewa kwa wana masumbwi (ngumi).
 
Pambano la masumbwi likiendelea.
Pambano la masumbwi likiendelea.
Afisa Uhusiano Mwandamizi wa PSPF, Abdul Njaidi, akiwa na Mkuu wa Kikosi Maalum cha Magereza jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari, wakati akitoa nasaha kwa wanamichezo kabla ya kuanza kwa bonanza hilo.
Nasaha za mgeni rasmi kwa wanamichezo.
Wanamichezo wakishangilia hotuba.
Onyesho la Judo.
Werema akimkabidhi sehemu ya vifaa hivyo vya michezo, Kocha na Afisa Michezo wa Kikosi Maalum cha Magereza Dar es Salaam, Inspekta Francis Tabu.
Soka likiendelea baina ya Kikosi Maalum na timu ya Magereza.
Mkuu wa Kikosi Maalum cha Jeshi la Magereza Ukonga jijini Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi wa Magereza, Rajabu Nyange Bakari.
Picha ya pamoja

JACQUELINE MENGI AUNGA MKONO JUHUDI ZA JPM KWA KUKARABATI NA KUNUNU VITABU VYA MAKTABA

 Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (wa pili kushoto) akiwa ameongoza na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda (kushoto), Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge (wa tatu kushoto) pamoja na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga mara baada ya kuwasili shuleni hapo.
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na wanafunzi wa Shule ya Msingi Kinondoni ambapo aliwahimiza kusoma kwa bidii vitabu hivyo ili kupanua ufahamu wao zaidi na hata kimasomo pia vitasaidia kuinua viwango vyao vya ufaulu.
 Mkurugenzi wa Dr.Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi na uongozi wa shule hiyo kwa pamoja wakiimba na wanafunzi wa shule ya Msingi Kinondoni.
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akizungumza na waandishi wa habari kwenye hafla ya uzinduzi wa maktaba ya vitabu aliyoipa jina la Dr. Ntuyabaliwe Foundation katika hatua za kumuenzi marehemu baba yake ambaye aliyemjengea misingi mizuri ya usomaji wa vitabu wakati wa makuzi yake
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation na Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akionyesha  wageni waalikwa picha mbalimbali za awali kabla ya kukarabati maktaba hiyo.

  Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa maktaba ya Shule ya Msingi Kinondoni jijini Dar es Salaam.  Wanaoshuhudia tukio hilo ni Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi (katikati) pamoja na Diwani wa Kata ya Mwananyamala, Songoro Mnyonge.
 Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda na Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi kwa pamoja wakizundua nembo ya taasisi hiyo.
 Mkurugenzi wa Dr. Ntuyabaliwe Foundation, Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi wakipeana mikono na Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda.
  Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akimwonyesha baadhi ya vitabu Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda vinavyopatikana katika maktaba hiyo.
Miss Tanzania 2000, Bi. Jacqueline Mengi akifurahi katika picha ya pamoja na baadhi ya walimu wa shule hiyo wakati akiondoka shuleni hapo.

Na Mwandishi wetu
Kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa kizazi cha sasa na baadae, Jacqueline Mengi kupitia Taasisi yake ya Dk. Ntuyabaliwe ameamua kuunganisha nguvu kwa serikali ya awamu ya tano iliyo chini ya Rais Magufuli kwa kusaidia kuboresha upatikanaji wa elimu bora kwa kufanya marekebisho ya maktaba katika shule ya msingi Kinondoni.
Akizungumza wakati wa kukabidhi msaada huo ambao uliambatana na uzinduzi wa Taasisi ya Dk. Ntuyabaliwe, Jacqueline amesaidia kufanya ukukarabati wa maktaba katika shule hiyo na kuweka vitabu ikiwa ni sehemu ya kumkumbuka baba yake Dk. Ntuyabaliwe kutokana na kupenda kwake kusoma vitabu.
Alisema baba yake alikuwa akiamini zaidi katika vitabu hivyo alipenda hata watoto wake wasome vitabu na anachokifanya yeye kwa sasa ni kuendeleza juhudi ambazo alikuwa akiifanya baba yake ya kuona watu wakisoma vitabu na matarajio yake ni kuona vitabu hivyo vikiwasaidia wanafunzi wa shule hiyo kuwaongezea uwezo wa kufaulu katika masomo yao ya darasani.
"Ndoto yangu ya muda mrefu leo imetimia, kila mtu ambaye alikuwa akimfahamu baba yangu Dk. Ntuyabaliwe alikuwa akifahamu kuwa alikuwa anapenda vitabu na hata sisi alituzoesha kusoma vitabu na hata kuanzishwa kwa taasisi hii ni sehemu ya kumkumbuka yeye,
"Naamini kuwa usomaji wa vitabu unaweza kumsaidia mtu kufika mbali hata kama sio katika elimu unaweza kumsaidia kwa jambo lingine hata katika maisha ... ndoto yangu ni kuona watanzania wote wanapenda kusoma kama baba yangu alivyokuwa anapenda kusoma vitabu," alisema Jacqueline.
Nae mgeni rasmi katika shughuli hiyo, Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Raymond Mapunda alisema sio jambo rahisi serikali kuweza kumaliza changamoto zote zilizopo na kupitia watu wenye moyo kama wa Jacqueline ambao wanaunga mkono juhudi za serikali kunaweza saidia upatikanaji wa elimu bora.
Alisema kupitia maktaba hiyo anaamini ipo siku kutatokea mtu ambaye atakuwa na msaada kwa Tanzania ambaye wakati akisoma alikuwa akitumia maktaba ambayo imefanyiwa ukarabati na Jacqueline Mengi.
"Nimeona hali ambayo ilikuwa awali katika eneo hili na niseme tu Jacqueline atakuwa na yeye aliguswa na hali hiyo na nitumie fursa hii kumshukuru sana kwa msaada ambao ameutoa, shule inatakiwa kutoa elimu bora lakini ili kufikia malengo hayo kunahitajika kuwe na nyenzo za kutosha ambazo zitasaidia malengo ya kielimu kufikiwa," alisema Mapunda.
Kwa upande wa Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kinondoni, Emmanuel Ntenga alimshukuru Jacqueline Mengi kwa msadaa wa kukarabati maktaba ya vitabu ili wanafunzi kujisomea, maktaba ambayo awali hawakuwahi kuwa nayo.
"Tunakushukuru sana kwa maktaba hii sasa wanafunzi wataweza kujisomea, tunafahamu juhudi za Dk. Mengi katika kusaidia elimu kwa kutoa madawati sasa na wewe umemuunga mkono tunawashukuru kwa hilo," alisema Ntenga.