Rubani wa ndege ndogo iliyoanguka
juu ya mti amelazimika kulala usiku juu ya mti na kusubiri kwa saa 12
baada ya waokoaji kusema inabidi wasubiri hadi pakuchwe ili
wamuokoe.
Rubani na ndege hiyo ilianguka na
kutua juu ya mti, karibu kilomita 30 mashariki mwa Mji wa Stuttgart
kusini mwa Ujerumani jumatatu usiku.
Waokoaji walihofia kufanya zoezi la
uokoaji usiku wa manane kwa kuogopa kuwa wakifanya hivyo huenda ndege
hiyo ikaanguka chini ya mti.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni