Wasanii
wa kijiji cha Katumba wilayani Mpanda wakicheza ngoma ya Kasimbo
wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadhara
kijijini hapo akiwa katika ziara ya mkoa wa Katavi Agosti 21, 2016.
(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri
Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary (kulia kwake) wakiwapungia
wananchi wa Mpanda wakati walipowasili kwenye uwanja wa Kashaulili
mjini Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara Agosti21, 2016. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wananchi
wakionyesha mabango wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipowasili
kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda kuhutubia mkutano wa hadhara
Agosti 21, 2016. Katika hotuba yake Waziri Mkuu alizitolea majibu kero
zote zilizoandikwa kwenye mabango hayo akiwahusisha watendaji wa
Halmashauri, mkoa na wilaya. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mke
wa Waziri Mkuu, Mama Mary Majaliwa akiwasalimia wananchi wa Mpanda
wakati Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipohutubia mkutano wa hadahara
kwenye uwanja wa Kashaulili mjini Mpanda Agosti 21, 2016. Kulia ni Mkuu
wa mkoa wa Katavi, Meja Jenerali Mstaafu, Raphael Mbuga. (Picha na Ofisi
ya Waziri Mkuu)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni