Na Stella Kalinga, Simiyu
Mkuu
 wa Mkoa wa Simiyu, Mhe.Anthony Mtaka ametoa ufafanuzi wa agizo la 
kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu 
Kata  mkoani humo,  ambalo Serikali ya Mkoa ililitoa tarehe 17 Agosti 
,2016 katika kikao ambacho alipokea  Vishikwambi (tablets) 637 kutoka 
EQUIP Tanzania (Mpango wa Kuinua Ubora wa Elimu Nchini)  kwa ajili ya 
Walimu wakuu na Waratibu wa Elimu Kata
Mkuu
 huyo wa Mkoa ametoa ufafanuzi huo kufuatia kuwepo kwa taarifa za 
upotoshaji wa agizo hilo kama ilivyoripotiwa na baadhi ya vyombo vya 
habari na mitandao ya kijamii., kuwa Mkuu wa Mkoa ametangaza kuwavua 
madaraka Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu Elimu Kata wote wa 
Mkoa huo; hali iliyopelekea baadhi ya Walimu wakuu na Waratibu kukosa 
ari ya kufanya kazi,  kwa kigezo cha kusubiri kuvuliwa madaraka.
Mtaka
 amesema Mkoa ulipokea taarifa za takwimu za wanafunzi hewa, vyumba vya 
madarasa, idadi ya walimu na idadi ya madawati, baada ya kupokea taarifa
 hizo ulionekana utofauti mkubwa wa takwimu hizo ndipo Serikali mkoani 
humo, ikaahidi kupitia mapungufu ya udanganyifu wa takwimu hizo kwa kila
 shule na kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kuwawajibisha Walimu wakuu 
na Wakuu wa Shule waliodanganya idadi ya wanafunzi.
Aidha,
 Mtaka amesema Mkoa wa Simiyu umepata bahati ya kuwa na Mradi wa EQUIP 
Tanzania ambao umewawezesha waratibu kupata pikipiki na posho, walimu 
wakuu wamepewa vishikwambi kwaa jili ya utunzaji wa takwimu, hivyo 
Serikali inao wajibu wa kuangalia mahitaji ya Mkoa katika elimu ambapo 
alielekeza yafanyike mabadiliko ya Walimu wakuu Msingi, Sekondari na 
Waratibu wa mkoa mzima.
Katibu
 wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema(kulia) akizungumza na Maafisa Elimu
 na Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha
 kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la 
kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo 
liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, 
kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka. 
“Nililisema
 mwanzo na leo nalirudia tutafanya mabadiliko makubwa kwa Wakuu wa Shule
 za Msingi, Sekondari na Waratibu Elimu kata kwa kujiridhisha na 
maendeleo ya shule zetu, idadi ya walimu waliopo,idadi ya wanafunzi, 
kiwango cha ufaulu wa wanafunzi na mazingira ya shule ; lakini tutatoa 
upendeleo kwa shule 10 bora katika kila wilaya kwa Mitihani ya Kitaifa 
ya Darasa la IV, VII Kidato cha II na IV , hiki ni kipimo kimojawapo cha
 walimu wa kuendelea nao. Nasisitiza hakuna mtu atakayeonewa wala 
kufedheheshwa”, alisema Mtaka.
Mtaka
 amesema azma ya Serikali ni kuibua vipaji vipya vya viongozi wa Elimu 
katika ngazi ya Wilaya ambapo alisema ameshaagiza Maafisa Elimu wa 
Wilaya kuwasilisha taarifa ya walimu waliojiendeleza katika ngazi 
shahada ya kwanza na shahada ya uzamili ili watakaokuwa na sifa waweze 
kuteuliwa katika nafasi za Walimu wakuu, Wakuu wa Shule na Waratibu 
Elimu Kata ambao watafanyiwa upekuzi (vetting) na Vyombo vya Ulinzi na 
Usalama.
Baadhi
 ya Wajumbe wakimsikiliza Mkuu wa Mkoa wa Simiyu (hayupo pichani) wa 
kikao maalum cha kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewwa na Serikali 
Mkoani humo la kufanya mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu 
kata, ambalo liliripotiwa tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya
 kijamii. kuwa Serikali imetangaza kuwavua madaraka. 
Sanjari
 na hilo , Mkuu huyo wa Mkoa amesema Walimu wakuu na Wakuu wa shule wa 
zamani ni tofauti na wale wa sasa,  kwa kuwa sasa hivi wamekuwa maafisa 
masuuli wa shule zao ambapo wanapokea fedha za Elimu bila malipo kupitia
 akaunti za shule zao, hivyo ni lazima wapatikane watu waadilifu, wenye 
sifa na uwezo wa kuongoza shule na kusimamia fedha za Serikali.
Akichangia
 katika kikao hicho Afisa Elimu  (Msingi) Wilaya ya Meatu, George Lowasa
 ameshauri Uchambuzi wa watu watakaoteuliwa ufanyike katika umakini 
mkubwa ili wapatikane watendaji wazuri na kuhusu utoaji wa takwimu 
sahihi alishauri kuwe na utaratibu wa kuziboresha kila (robo) baada ya 
miezi mitatu ili kuwa na takwimu sahihi pale zinapohitajika.
Kwa
 upande wake Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amesema Uteuzi
 huo utazingatia sheria, kanuni, taratibu na miongozo ya uteuzi ambapo 
hakuna mtu atakayeonewa au atakayependelewa.
Wakati
 huo huo Mkuu wa Mkoa amesema atawachukulia hatua Maafisa wale 
wanaolalamikiwa na walimu kwa kuwatolea lugha mbaya  kila wanapotoa 
huduma kwa walimu hao katika Halmashauri za Mkoa huo.
Katibu
 Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini akizungumza na Maafisa Elimu na 
Viongozi wa CWT wa Mkoa huo (hawapo pichani) katika kikao maalum cha 
kutoa ufafanuzi wa agizo lililotolewa na Serikali Mkoani humo la kufanya
 mabadiliko ya Walimu wakuu na Waratibu Elimu kata, ambalo liliripotiwa 
tofauti katika vyombo ya habari na mitandao ya kijamii, kuwa Serikali 
imetangaza kuwavua madaraka.
Naye
 Katibu wa CWT Mkoa wa Simiyu, Said Mselema ameshauri  baada ya 
mabadiliko ya wakuu wa shule na Waratibu wa Elimu Kata kufanyika wale 
ambao wataonekana hawana sifa za kuendelea kushika nafasi hizo 
waondolewe kwa staha, ambapo aliomba Serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa 
ikishirikishe chama hicho katika masuala yote muhimu ya kuendeleza sekta
 ya Elimu, kwa kuwa wanamsaidia mwajiri katika usimamizi wa utendaji kwa
 walimu.
Kikao
 hicho cha wadau kilichofanyika mjini Bariadi na  kimewahusisha Wajumbe 
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, Maafisa Elimu kutoka Halmashauri  
zote za Mkoa wa Simiyu pamoja na  Wenyeviti na Makatibu wa Chama cha 
Walimu Tanzania (CWT) ngazi ya  Mkoa na Wilaya.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni