Katibu wa UVCCM mkoa wa Arusha Ezekiel Mollel akiwa anaongea na waandishi wa habari nje ya ofisi za umoja huo 
 mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya akiwa anaongea na waandishi wa habari mwenyekiti wa UVCCM wialaya ya Arumeru Boniface Mungaya akichangia jambo katika mkutano huo ambapo alisema kuwa watakuwa bega bega viongozi hao kuakikisha mali za umoja huo silizotaifishwa zitarudishwa ,wakwepa kodi watalipa au kufukuzwa na maduka yote yanapangishiwa wananchi wa CCM ili wanufaike
Kamanda wa UVCCM Philemoni Monaban akiongea na waandishi nae alisema kuwa anawaunga mkoano vijana hawa na atakuwa nao bega kwabega
mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha Lengai Ole Sabaya akiteta jambo na kamanda wa UVCCM
Na Mahmoud Ahmad,Arusha
 UMOJA  wa vijana mkoa wa Arusha UVCC, umetoa siku 14 kwa wapangaji
wote waliokiuka kulipa kulipa kodi za pango la miradi ya umoja huo na
endapo watakaidi amri hiyo ya kulipa kodi hizo hatua kali
zitachukuliwa ikiwa ni pamoja na kuwafikisha mahakamani.
Akiongea na vyombo vya habari Mara baada ya kumalizika kwa kamati ya
utekelezaji mapema  katibu wa Umoja huo Ezekieli Molel alisema
kuwa wapo baadhi ya viongozi ambao wanahusika kuhujumu miradi ya Umoja
huo na kisha kulipwa kama wamiliki halisi wa majengo na miradi  ya
Umoja huo.
Alisema kuwa miradi inatakiwa kuingiza kiasi cha milioni zaidi ya 20 kwa mwezi 
lakini kitu cha ajabu miradi hiyo inaingiza kiasi cha milioni tatu
pekee kwa mwezi
Alidai kuwa kinachotokea ni kwamba wapo wapangaji ambao wanalipa kodi
kwa kiasi cha 5000 kwa mwezi kwa kuwa wanafahamina na wamiliki
waliojiandikishia mkataba hali amabyo inawafnya wengine kujinufaishia
juu ya migongo ya umoja huo
"Tunalagaiwa sana alafu hawa wapangaji wetu wanatupa shida alafu Mkuu
wa mkoa anawatetea baadhi yao kwa kusema kuwa tuwaache kweli jamani
tupokee kodi 5000 hatukubali kabisa na wengine wamekaa muda mrefu lakini
 hawalipi kweli ni haki hapana atutakubali tutakula nao sahani 
moja"aliongeza molel
Kwa upande wake mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Arusha  Lengai Ole Sabaya alisema kuwa  kuna taarifa zinaonesha kuwa aliyewahi kuwa
katibu wa Umoja huo ambaye ni mfaume kizigo(naibu katibu Mkuu
bara)alihusika kwa namna moja kudidimiza uchumi wa  umoja huo.
Kutokana na hali hiyo mwenyekiti  huyo alimtaka naibu katibu Mkuu kurudi
Arusha na kisha kuweza kuangalia makubaliano ambayo aliingia na
wapangaji wakati alipokuwa  katibu wa vijana mkoani hapo
"kuna vigogo ambao kwa kuwa wana majina ndani ya chama wanarubuni mali
za chama kabisa sasa hatutakubali kabisa hata kama wapo ngazi za juu
ni lazima tuhakikishe tunawatoa"aliongeza Ole sabaya 
Kutokana na hilo alisema wametoa siku 14 kwa wapangaji ambao
wanahujumu miradi ya chama hicho kujisalimisha na kisha kulipa madeni
yote na endapo kama watashindwa kufanya hivyo watafakisha mahakamani.
Aidha
 aliongeza kuwa kama kunampangaji yeyote aliyepangisha duka 
alilokabidhiwa na umoja wa vijana nae akapangisha kwa mtu mwingine 
yeyote hata kama ni kiongozi ndani ya chama amekosa sifa za kuwa 
mpangaji kwa mujibu wa makubaliano ya mkataba na toka sasa hatambuliki 
tena .  
 Ole 
 Sabaya aliongeza kuwa wao kama umoja wa vijana mkoa wa Arusha  
wanalaani vikali matamshi ya mbunge wa Arusha Mjini  Godbless Lema na 
viongozi wake kwa ujumla kwa kuingilia mamlaka halali ya mkuu wa wialya 
ya Arusha mjini Mrisho Gambo ya kutaka kujua uhalali wa fedha 
wanazolipwa madiwani kinyemela huku wananchi wa jiji wakiendelea kupata 
dhiki ya maji ,afya pamoja na miundo mbinu
Walimtaka
 mkuu wawilaya aendelee na kazi bila ya woga wala hofu huku akimfundisha
 mbunge huyo kufata mipaka ya kazi yake na kukumbuka kwamba kazi 
aliy9oomba sio ya kunufaisha matumbo ya madiwani wake bali ni ya 
kuwapunguzia wana nchi wa Arusha ukali wa maisha.  
Katika hatua nyingine akiongea kwa njia ya simu  naibu katibu mkuu wa
UVCCM taifa, mfaume kizigo alisema kuwa tuhuma hizo ni za uongo kabisa
nay eye hausiki na mkataba wowote kwani kwa mujibu wa sheria za CCM
mikataba yote inafanyika na kuna kuwa na uwazi
Alidai kuwa hana mali yoyote ambayo ameihujumu na hivyo hao vijana
kama wangekuwa na malalamiko basi wangeyafikisha kwenye uongozi ngazi
za juu.
Hataivyo jitiada za kumtafuta Mkuu wa mkoa wa Arusha daudi Ntibenda zinaendelea.






Hakuna maoni:
Chapisha Maoni