Mwanariadha
Usain Bolt aliyetangaza kutoshiriki tena michuano ya Olimpiki,
ameweka rekodi kwa kupata ushindi wa medali tatu za dhahabu na ya
tisa katika michuano hiyo wakati Jamaica ikishinda mbio za kupokezana
vijiti watu wanne Jijini Rio.
Kabla
ya ushindi huo Bolt, 29, alishashinda medali za dhahabu katika mbio
za mita 100, na 200, na sasa amekuwa mwanariadha pekee mwanaume
kushinda medali tatu za dhahabu mfululizo katika michuano mitatu ya
michezo ya Olimpiki.
Bolt
alishirikiana na Asafa Powell, Yohan Blake na Nickel Ashmeade ambapo
walimaliza kwa kutumia sekunde 37.27. Katika mbio hizo Japan
walishangaza ulimwengu kwa kutwaa medali ya fedha na Canada shaba.
Mwanariadha wa Jamaica Usain Bolt akikatiza katika mstari wa kumaliza mbio hizo
Wanariadha wa Jamaica Usain Bolt, Asafa Powell, Yohan Blake na Nickel Ashmeade wakifurahia ushindi wao
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni