Usiku
wa jana Ijumaa Agost 19,2016 kuamkia leo Jumamosi Agost 20,2016,
kulikuwa na mtifuano mkali wa kumtafuta mlimbwende wa taji la MISS
MWANZA 2016 ambapo warembo 16 kutoka wilaya mbalimbali mkoani Mwanza
walijitosa kusaka taji hilo.
Ilikuwa
ni furaha kubwa kwa mrembo, Mary Peter (katikati), pale alipotangazwa
kuwa MISS MWANZA 2016. Pia mwendelezo wa furaha uliwaendea warembo,
Victoria Boniphace (kushoto) aliyetangazwa Miss Mwanza nambari mbili na
Winnie Shayo (kulia), aliyetangazwa Miss Mwanza nambari tatu.
Kinyang'anyiro
cha Miss Mwanza 2016, kiliandaliwa na Kampuni ya "Big D Entertainment"
na baada ya kinyang'anyiro hicho, unafuata mtifuano wa MISS LAKE ZONE
2016 utakaofanyika Septemba 10,2016 ambapo washiriki wa Miss Mwanza 2016
waliongia nafasi tano bora, wanashiriki moja kwa moja kwenye shindano
hilo.
Na BMG
Miss
Mwanza 2015, Donny Roberty (kushoto), akimkabidhi taji Miss Mwanza
2016, Mary Peter (kulia) baada ya kuibuka mshindi wa shindano hilo.
Washiriki wa Miss Mwanza, walioingia nafasi tano bora
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016.
Warembo walioshiriki Miss Mwanza 2016
Majaji walikuwa na Kazi pevu kuchagua mshindi
Baadhi ya waliohudhuria kwenye tukio
Msanii Elizayo HB kutoka Jijini Mwanza akidondosha burudani kwenye Miss Mwanza 2016
Burudani za kiafrika pia zilikuwepo
Mkali wa Moyo Mashine, Ben Pol, alidondosha burudani poa sana
Ben Pol kazini
Kupitia
BMG, Ben Pol, aliwashukuru wakazi wa Jiji la Mwanza kwa namna
wanavyopenda kazi zake na kuahidi kufanya kazi nzuri zaidi.
Miss
Mwanza 2016 aliiambia BMG kwamba, maandalizi yake mazuri ndiyo
yaliyompa fursa ya kunyakua taji hilo na kwamba amejiandaa vyema kwa
ajili ya taji la Miss Lake Zone 2016 na pia Miss Tanzania 2016.
Miss
Mwanza 2016 nambari mbili akibonga na BMG. Anasema shauku yake ni
kuongeza juhudi zaidi ili kunyakua taji la Miss Lake Zone 2016.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni