Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe
17 Agosti, 2016 amekutana na kufanya mazungumzo na Kiongozi Mkuu wa
Jumuiya ya Dawoodi Bohra Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin
Saheb(TUS) Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo
hayo yamehudhuriwa na Mufti wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ali na
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Augustine
Mahiga ambapo Rais Magufuli ameipongeza Jumuiya ya Dawoodi Bohra kwa
juhudi kubwa inazofanya katika kutoa huduma za kiroho na pia kushiriki
katika maendeleo.
Dkt.
Magufuli amewakaribisha wana Jumuiya hiyo kuwekeza hapa nchini hususani
katika sekta ya viwanda na pia amewakaribisha katika Maadhimisho ya
Jumuiya ya Dawoodi Bohra duniani yanayotarajiwa kufanyika Jijini Dar es
Salaam Mwezi Oktoba 2016.
"Tanzania
ni nchi nzuri, tumekuwa na ushirikiano mzuri sana na wenzetu wa Jumuiya
ya Bohra, hivyo njooni mfanye biashara na Tanzania, tumepanga katika
kipindi cha mwaka 2016/2017 hadi 2020/2021 Tanzania iwe nchi ya viwanda,
kwa hiyo tunawakaribisha kuja kuanzisha viwanda vya kutosha" Amesema Rais Magufuli.
Kwa
upande wake Kiongozi Mkuu wa Jumuiya ya Dawoodi Bohra Mtukufu Dkt.
Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb amempongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri
inayofanywa na Serikali yake ya awamu ya Tano, na pia ameahidi kuwa
Jumuiya ya Dawoodi Bohra ipo tayari kushirikiana na Tanzania katika
maendeleo.
Aidha,
Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Saheb amemkabidhi Rais Magufuli
hundi ya Dola la Marekani Elfu Hamsini na Tatu (USD-53,000) sawa na
Shilingi Milioni 116 za Kitanzania kwa ajili ya kuchangia utengenezaji
wa madawati ya wanafunzi kwa shule mbalimbali hapa nchini na pia
amekabidhi hundi ya Dola za Marekani Elfu Ishirini na Moja (USD-21,000)
sawa na Shilingi Milioni 46 kwa ajili ya Baraza Kuu la Waislamu Tanzania
(BAKWATA).
Katika hatua nyingine,
Rais Magufuli amepokea barua kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya
Saharawi Mhe. Brahim Ghali iliyowasilishwa na Mjumbe Maalum wa Rais huyo
ambaye ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mhe. Bachir Moustapha
Sayed.Pamoja na kupokea barua hiyo Rais Magufuli amesema Serikali yake
ya Awamu ya Tano itaendeleza na kuimarisha zaidi ushirikiano wake na
Jamhuri ya Kiarabu ya Saharawi na pia itaendelea kuunga mkono juhudi za
wananchi wa Saharawi kupata haki ya kuamua hatma yao.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es Salaam
17 Agosti, 2016.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wakwanza kushoto.(Katikati ni mkalimani)
Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin akimuombea dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuchangia madawati kwa kutoa hundi yenye thamni ya dola za Kimarekani (USD 53,000) kwa ajili ya utengenezwaji wa madawati.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimshukuru Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kuchangia madawati kwa kutoa hundi yenye thamni ya dola za Kimarekani (USD 53,000) kwa ajili ya utengeezwaji wa madawati. Wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir watatu kutoka kushoto na Sheikh mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Alhadi Mussa Salum wa kwanza kushoto.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir pamoja na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Dkt. Augustine Mahiga pamoja na viongozi wengine wa BAKWATA na wa madhehebu ya Bohora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin wengine katika picha ni Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir pamoja na viongozi wengine wa Madhehebu ya Bohora.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akijadiliana jambo na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin kabla ya kuondoka Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin mara baada ya kumaliza mazungumzo yao Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Mufti Mkuu wa Tanzania Sheikh Aboubakar Zubeir Ikulu jijini Dar es Salaam mara baada ya kuagana na mgeni wake Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Kiongozi Mkuu wa Madhehebu ya Bohora Duniani Mtukufu Dkt. Syedna Mufaddal Saifuddin aliyeambatana na ujumbe wake Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. John Pombe Magufuli akipokea ujumbe uliotoka kwa Rais wa Saharawi na kuwasilishwa kwake na Mjumbe Maalum Bachir Moustapha Ikulu jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU.

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni