Katibu wa
Uvccm mkoa wa Arusha Ezekiel Mollel amesema kuwa umoja huo utaendelea na
kuingia mikataba mipya na wapangaji wake waliondani ya vibanda na si vingine.
Kauli hiyo
ameitoa leo wakati akiongea na wanahabari ofisini kwake ambapo alikumbushia siku
14 walizotoa kwa wapangaji hao wa umoja huo wa vijana kuwa zimeisha na yeyote
atakaekadi hatua zitachuliwa.
Mollel alisema
kimsingi wamekubaliana kuingia mkataba mipya na wapangaji wote kwenye vibanda
49 vinavyomilikiwa na umoja huo kwa wapangaji kuingia mkataba wa mwaka mmoja mmoja.
Akatanabaisha
kuwa na wale wapangaji waliowapangishia hapo mwanzo nao kuwapangishia waliomo
wao hawatawatambua na kuanzia mwezi ujao wataanza zoezi la kuingia mikataba
mipya.
Aliwataka
wapangaji hao kufuata maelekezo waliokubaliana kwenye kikao chao na wale
walipangishia wengine watakuwa wamejiondoa wenyewe huku aliendani ndie
wataingia nae mkataba mpya.
“Hiki
kibanda no 46 tumekubaliana na mpangaji aliekuwepo ambaye tulimfungia kuendelea
na biashara na huyo na mmliki wa awali sisi hatumtambui kwa teyari ameshajilipa
mwenyewe”alisema Mollel.
Aidha
akizungumzi eneo la Barcelona lenye eka mbili ambalo pia linamilikiwa na umoja
huo alisema kuwa wametangaza zabuni za upangaji wa eneo hilo na atakayeshinda
zabuni ndio ataendesha eneo hilo
.
Nae
mwenyekiti wa umoja huo mkoani hapa Lengai ole Sabaya alisema kuwa suala la
nyumba za umoja huo ambayo katibu aliekuwepo huko nyuma Kizigo alijiuzia kwa
kiasi cha 3 milion kwenye eneo la Ngarenaro ataalipeleka ngazi za juu kwa
maamuzi zaidi.
Wiki mbili
zilizopita Uvccm mkoani hapa walitoa tamko lao mbele ya waandishi wa habari
ambapo alikemea vikali mikataba iliyoingia ya upangishaji wa vibanda vya umoja
huo na kujikuta wakiwa hawana kitu huku fedha zikichuliwa na wapangaji wao kwa
mikataba minono ya 450,000 huku umoja huo ukiambulia 5000 kwa kibanda namba 46
haliiliyopekea kuingia na sera mpya ya mikataba ya vibanda hivyo
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni