Zoezi la upigaji kura za urais na
ubunge limeanza nchini Zambia baada ya kumalizika kwa kampeni
zilizokabiliwa na mapambano baina ya wafuasi wa vyama vinavyokinzana.
Uchaguzi huu unatarajiwa kuwa ni wa
upinzani mkali baina ya rais Edgar Lungu wa chama cha PF na mgombea
wa upinzani wa chama cha UPND, Hakainde Hichilema.
Kwa mara ya kwanza, mgombea wa urais
nchini humo atalazimika kushinda kwa zaidi ya asilimia 50 ya kura
zote, ili kuepuka uchaguzi wa marudio.
Rais Edger Lungu akihutubia katika moja ya mikutano ya kampeni
Mgombea urais wa chama cha upinzani Hakainde Hichilema
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni