Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akifafanua jambo katika
mkutano na wachimbaji pamoja na watumiaji wa makaa ya mawe (hawapo
pichani) uliojadili changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo. Mkutano
huo ulifanyika Agosti 24, mwaka huu, Makao Makuu ya Wizara, jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini, Profesa
James Mdoe.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Madini,
Profesa James Mdoe, akizungumza na wachimbaji pamoja na watumiaji wa
makaa ya mawe (hawapo pichani), wakati wa Mkutano baina yao na Waziri wa
Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (hayupo pichani). Mkutano
huo ulifanyika hivi karibuni, Makao Makuu ya Wizara hiyo jijini Dar es
Salaam.
Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (kushoto) na Naibu
Katibu Mkuu anayeshughulikia Madini, Profesa James Mdoe (kushoto kwa
Waziri), wakifuatilia majadiliano yaliyokuwa yakiendelea wakati wa
Mkutano baina ya Wizara na wachimbaji pamoja na watumiaji wa makaa ya
mawe, uliofanyika Agosti 24 wizarani, jijini Dar es Salaam.
Wajumbe
mbalimbali walioshiriki Mkutano baina ya Waziri wa Nishati na Madini,
Profesa Sospeter Muhongo na Wachimbaji pamoja na Watumiaji wa Makaa ya
Mawe, wakifuatilia mijadala mbalimbali katika Mkutano huo uliofanyika
Agosti 24 mwaka huu Makao Makuu ya Wizara jijini Dar es Salaam.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni