Sasha
Obama, binti wa rais wa Marekani Barack Obama, ameacha kwa muda
kudeka Ikulu na kufanya kazi ya uhudumu kwenye kaunta ya hoteli ya
vyakula vya baharini.
Shasha
mwenye miaka 15 amechukua kibarua cha muda katika majira ya joto kwa
sasa katika eneo la biashara huko Martha's Vineyard, Massachusetts.
Sasha,
anatumia jina lake kamili la Natasha, amekuwa akisindikizwa kwenda
kufanya kazi kwenye hoteli hiyo na walinzi wa rais sita kwa mujibu wa
Boston Herald.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni