


Mkuu wa Wilaya ya Arusha Mrisho Gambo akiwa anatoa utambulisho kwa viongozi mbalimbali waliohudhuria sikubyaufunguzi wa.maonusho ya wakulima na wafugaji yanayondelea katika viwanja vya Themi Njiro.
NaMahmoud Ahmad,Arusha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Daud Filex Ntibenda amewataka Wakurugenzi wote wa Mikoa yote mitatu iliyopo Kanda ya Kaskazini ,wabadilishe mabanda yao na wajenge ya kisasa zaidi kwaajili ya maonyesho ya wakulima na wafugaji ambayo yatakuwa na mvuto zaidi.
Aliyasema hayo alipokuwa kifungua maonyesho ya nanenane yanayoendelea katika viwanja vyaThemi nanenane Njiro Jijini Arusha,huku akiwataka Taso washirikiane na Jiji pamoja na viongozi wa mikoa yote ili waweze kutengeneza ukumbi mkubwa wa kisasa.
Aidha alisema kumekuwa na changamotoya wananchi.kutoielewa kauli mbiu ya maonyesho ya nanenane mwaka huu hivyo basi amewaagiza wakulima na wafugaji waweze kuingia.kwenye mafunzo ya shamba darasa na kwenye mabanda ili waweze kupata elimu zaidi.
Aliwaagiza washiriki wenye mabanda yenye technolojia za kilimo waandae taarifa fupi ambayo mwananchi atakwenda nayo nyumbani na zitakazo waletea mabadiliko katika maeneo wanayotokea.
Sambamba na hayo aliwataka Taso kuangalia sheria viwanja vya maonyesho ambayo inapiga marufuku ongezeko la makazi ndani ya viwanja vya maonyesho,pia amewataka washiriki wote wa maonyesho watoe ushirikiano kwa vyombo vyabulinzi na Usalama na katika maeneo yao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni