Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla amefanya ziara ya kikazi katika Zahanati na vituo vya
Afya katika Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara ambapo ametoa maagizo
mbalimbali yafanyiwe kazi huku suala la watumishi likibainika kuwa ni
tatizo katika Wilaya hiyo.
Naibu
Waziri wa Afya Dk. Kigwangalla aliweza kutembelea Zahanati ya Hunyari
iliyopo Kijiji cha Hunyari, Zahanati ya Kihumbu, Maliwanda, Kituo cha
Afya Mugeta, Zahanati ya Sanzate, Kituo cha Afya Ikizu.
Aidha,
amewataka watendaji na Halimshahuri hiyo kuhakikisha wanakamilisha
maboresho na utekelezaji mwingine ikiwemo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya
kupanga safu ya ufanyaji wa kazi kwa kuwapeleka watalaamu katika
Zahanati hizo ili kuwahudumia wananchi walio pembezoni.
Kwa
upande wake, Mbunge wa Jimbo la Bunda Vijijini, Mh. Boniface alipongeza
ziara hiyo kwani wameweza kubaini changamoto mbalimbali zinazoikabili
sehemu ya utoaji wa huduma za Afya hivyo ujio wake huo kwenye maeneo
hayo ya Vijijini yamewafungua macho.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akitembelea kukagua shughuli za ufanyaji kazi wa
Zahanati ya Hunyari
Jengo maalum la wodi ya Wazazi la Zahanati ya Hunyari ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo kutoka Mkurugenzi wa Wilaya ya
Bunda namna watakavyoisaidia Zahanati hiyo
Mbunge
wa jimbo la Bunda Vijijini, Mh.Boniface Mwita Getere akimtambulisha
Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh.
Dk. Hamisi Kigwangalla pamoja na viongozi wengine akiwemo Mkuu wa Wilaya
ya Bunda Bi.Lydia Simeon Bupilipili.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akitoa maelezo na kupongeza wananchi wa kuweza
kuchangia juhudi za ujenzi wa jengo la wodi la akinamama, Kulia ni Mkuu
wa Wilaya ya Bunda Bi.Lydia Simeon Bupilipili.
Moja
la jengo la Zahanati ya Kihumbu ambalo nalo mejengwa kwa nguvu ya
wananchi kama linavyoonekana ambalo Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla aliweza
kulitembelea kukagua ujenzi wake.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Bunda,
Dk. Jonathan Ezekiel Budenu ( Wa tatu kulia) afanyie haraka marekebisho
ya upungufu wa wafanyakazi hasa maeneo ya vijijini.
Mbunge
wa jimbo la Bunda Vijijini, Mh.Boniface Mwita Getere akielezea jambo
kwa wananchi wa Kijiji cha Mugeta wakati Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo
ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla
alipotembelea kituo hicho cha Mugeta.
Moja ya jengo la Zahanati ya Sanzate ambalo limejengwa kwa nguvu za wananchi kama linavyoonekana pichani.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikagua jengo hilo la Sanzate ambalo limejengwa kwa
nguvu za wananchi.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akitoa maagizo kwa watendaji wa kijiji cha Sanzate.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akiwasili kijiji cha Makongoro kukagua Kituo cha Afya
Ikizu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akiwaonyesha bomba linalotakiwa kuwekwa katika chumba
cha upasuaji wakati wa kuingia kwenye chumba cha upasuaji.
msafara ukiendelea.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akipatiwa maelezo namna mashine kubwa ya kisasa ya
ufuaji nguo ambayo ilitolewa na Wizara ya Afya ambayo hata hivyo Kituo
hicho wameshindwa kuifanyia kazi.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akionyeshwa moja ya majokofu ya kuhifadhia mahiti
kwenye kituo cha Afya Ikizu.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akikabidhi Wheel chair kwa ajili ya wagonjwa wa kituo
cha Afya cha Ikizu ambapo Mbunge wa jimbo hilo, Mh. Boniface Getere
alizitoa kama mchango wake.

ukaguzi ukiendelea
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akiaga wakati alipotembelea kwa karakana ya uchongaji
ambayo ina historia ndefu.
eneo la karakana ambayo ina historia ndefu ambapo jengo hilo ndipo palipochongwa kifimb cha Hayati Mwalimu Julius Nyerere.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mh. Dk.
Hamisi Kigwangalla akiwa pamoja na viongozi wa Wilaya hiyo ya Bunda
wakati wa kumaliza ziara hiyo ya kutembelea vituo vya Afya katika Wilaya
ya Bunda.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni