Waziri
wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira,January Makamba
akifungua warsha ya wadau wa kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa
Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya
Tabia ya Nchi uliofanyika jana kwenye ukumbi wa Veta mjini Tanga kulia
ni Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais
anayeshughulikia pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi na
kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga,Mhandisi Zena Saidi
Kaimu
Mkurungenzi wa Mazingira kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais anayeshughulikia
pia mabadiliko ya tabia ya Nchi, Richard Muyungi akizungumza katika
warsha hiyo ya siku mbili inayofanyika kwenye ukumbi wa Veta Mkoani
Tanga.
Baadhi
ya washiriki wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya Taarifa ya Mchango wa
Tanzania katika Juhudi za Kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya
Tabia ya Nchi katika kikao kilichofanyika kwenye ukumbi wa Veta Jijini
Tanga wakimsikiliwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na
Mazingira,January Makamba alikuwa akifungua mkutano huoTANZANIA
inatarajiwa kutumia takribani dola mil500 hadi ifikapo mwaka 2030 ili
kuweza kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi yanayoendelea
katika maeneo mbalimbali hapa nchi.Kiasi hicho cha bajeti kinatarajiwa
kutumika kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo itasaidia
kupunguza juhudi za kupunguza joto zinazosababishwa na mabadiliko ya
tabia nchi.Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira January Makamba wakati wa ufunguzi wa warsha ya wadau kuhusu ripoti ya taarifa ya mchango wa Tanzania katika juhudi za kimataifa za kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Aliitaja baadhi ya miradi ambayo itatekelezwa ili kupunguza gesi joto hapa nchini kuwa ni dampo la mtoni katika Jiji la Dar Es Salaam,miradi ya nishati jadidifu katika maeneo ya Mbinga,Makete,Njombe Usa River na Ifakara.
“Miradi hiyo yote inajumla ya megawati tano(5MW) za uzalishaji wa hewa ukaa ambapo iwapo hatua za haraka hazitaweza kuchukuliwa athari za kimazingira zinaweza kuendelea kujitokeza”alisema Waziri Makamba.
Ambapo alisema katika kushiriki juhudi za kimataifa za kupunguza uzalishaji wa gesi joto tayari serikali ya Tanzania imeshaanza kutoa fursa kwa wadau ya kushughulikia mabadiliko ya tabia nchi .
Makamba alisema kuwa mikakati hiyo kwa sasa imeshaanza kutekelezwa katika ngazi za mikoa wilaya pamoja na Halimashauri mbalimbali hapa nchini.
“Juhudi za serikali ni kuhimiza matumizi ya gesi asilia katika uzalishaji wa nishati ya umeme yanaongezeka ili kuweza kupunguza matumizi ya vifaa vinavyozalisha hewa ukaa ili kukabiliana na kasi ya mabadiliko ya tabia nchi”alisisitiza Waziri Makamba.
Kwa upande wake Kaimu Mkurungenzi wa Mazingira kutoka wizarani Richard Muyungi alisema kuwa sasa wapo kwenye mkakati wa kutoa elimu kwa wadau wa mazingira kwenye kanda mbalimbali nchini.
Alisema ilikuweza kuwa na mipango madhubuti katika utekelezaji mkakati wa taifa wa mawasilinao wa mabadiliko ya tabia nchi kupitia wizara za kisekta.
Habari kwa Hisani ya Blog ya Kijamii ya Tanga Raha
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni