Mwanariadha
wa Kenya Vivian Cheruiyot ameshinda mbio za mita 5,000 na kumshinda
Ayana Almaz wa Ethiopia ambaye alikuwa wakitarajiwa kushinda mbio
hizo lakini akaishia kupata medali ya shaba.
Almaz,
24, alishinda mbio za mita 10,000 na kuweka rekodi wiki iliyopita na
alitarajiwa kushinda pia mbio hizo za mita 5,000 ili kutwaa medali
mbili za dhahabu katika michuano ya Olimpiki Jijini Rio.
Hata
hivyo bingwa huyo wa dunia wa mbio za mita 5,000 alipitwa na
Cheruiyot katika mita 2,000 pamoja na mwanariadha mwingine wa Kenya
Hellen Onsando Obiri, aliyeshinda medali ya fedha.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni