Gwaride la wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na maafisa
 wa Hifadhi za Taifa likiingia katika viwanja vya mazoezi katika kambi 
ya mafunzo ya Mlele wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi akipokea salamu ya utii kutoka kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya
Hifadhi ya Ngorongoro (hawapo pichani) wakati wa ufungaji  mafunzo kwa
askari na maafisa hao yaliyofanyika katika kambi ya mafunzo ya Mlele
mkoani Katavi  
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii
Meja Jenerali Gaudence Milanzi akikagua gwaride wakati wa kufunga mafunzo kwa askari wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) na
Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro yaliyofanyika katika kambi
ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi  
 Askari
 na Maafisa wa Hifadhi wakipita kwa heshima mbele ya mgeni rasmi  kwa 
mwendo wa pole na haraka wakati wa ufungaji  wa mafunzo ya kijeshi
waliyopata katika kambi ya mafunzo ya Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya
kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii
kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu kutoka mfumo wa kiraia.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja
Jenerali Gaudence Milanzi(kushoto) pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la
Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi wakipokea salamu za heshima kwa kupiga
saluti wakati gwaride likipita mbele kwa heshima wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari wa shirika la
Hifadhi za Taifa,(TANAPA) na Maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya taifa Ngorongoro.
 
 Bendi ya Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikipita mbele ya mgeni 
rasmi (hayupo pichani) wakati wa ufungaji wa mafunzo ya kijeshi kwa 
askari na maafisa wa Hifadhi ,Mafunzo yaliyofanyika katika kambi ya 
Mlele mkoani Katavi.
Askari
na Maafisa wa Hifadhi za Taifa wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati
wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya
Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
 
 Mkurugenzi
 wa Rasilimali watu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Witness Shoo
 (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Uhifadhi Mtango Mtahiko 
wakifuatilia maonesho ya matumizi ya silaha kutoka kwa wahitimu hao.
 Meneja Mawasiliano wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Pascal Shelutete akisherehesha wakati wa ufungaji wa mafunzo  ya kijeshi kwa askari
na Maafisa wa Hifadhi  waliyopata katika kambi ya
Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
Askari
na Maafisa wa Hifadhi wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati
wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya jeshi ya
Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
 Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence 
Milanzi,Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan 
Kijazi pamoja na Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro 
,Freddy Manongi wakifuatilia maonesho hayo. 
Askari
na Maafisa wa Hifadhi wakionesha umahiri katika matumizi ya silaha wakati
wakionesha kwa vitendo mafunzo ya kijeshi waliyopata katika kambi ya
Mlele mkoani Katavi ikiwa ni sehemu ya kubadili utendaji kazi wa taasisi zilizo
chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii kuendeshwa katika mfumo wa jeshi usu.
 
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitizama
matundu ya risasi zilizolengwa na mmoja wa askari wa uhifadhi waliohitimu
mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.Kulia kwake ni
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi. 
 Wakufunzi wa Mafunzo ya kijeshi kwa maofisa na askari wa Hifadhi za Taifa wakitambulishwa mbele ya mgeni rasmi,(hayupo pichani). 
 Mhifadhi
 kutoka Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro Lilian Magoma akisoma risala 
kwa niaba ya wahitimu wenzake wa mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika katika
 kambi ya Mlele iliyopo mkoani Katavi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii Meja Jenerali Gaudence Milanzi akitunuku vyeti kwa askari na maafisa wa uhifadhi waliohitimu
mafunzo ya kijeshi katika kambi ya Mlele mkoani Katavi.
 Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) Getrude Lyatuu akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo. 
 Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya  Ngorongoro,Freddy Manongi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo. 
 Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori Alexander Songorwa akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA)Allan Kijazi akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo hayo. 
 Mkurugenzi
 Mkuu wa Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) Allan Kijazi akimkaribisha
 Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence 
Milanzi kuzungumza na wahitimu wa mafunzo ya kijeshi kwa askari na 
maofisa wa Hifadhi za Taifa . 
 Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi 
akizungumza wakati wa ufungaji wa mafunzo kwa askari na maofisa wa 
Hifadhi za Taifa. 
 Katibu
 Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence Milanzi na
 viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na Utalii 
wakiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro 
  Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii,Meja Jenerali Gaudence 
Milanzi na viongozi wa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Maliasili na 
Utalii wakiwa katika pichaya pamoja na wahitimu wa mafunzo ya kijeshi yaliyofanyika katika kambi ya Mlele mkoani Katavi. 
Na Dixon Busagaga wa Michuzi Blog, Kanda ya Kaskazini. 

 
 

 




 
 

 

Hakuna maoni:
Chapisha Maoni