Rais Dkt.John Pombe Magufuli amesema kwamba serikali haina mpango wa
kuiuza Ikulu ya Rais jijini Dar es salaam kama ambavyo baadhi ya watu
walisema kufuatia utekelezaji wa mpango wa serikali kuhamia Dodoma.
Akizungumza kwenye ofisi ndogo ya CCM jijini Dar es salaam leo akitokea
mkoani Mwanza Rais Magufuli amesema kwamba mpango wa serikali kuhamia
Dodoma uko pale pale ikiwa ni ahadi yake mara baada ya kuchaguliwa kuwa
Mwenyekiti wa CCM mkoani Dodoma mwezi uliopita.
Rais Magufuli alisema serikali pamoja na watumishi wote wa watahamia
Dodoma ila Ikulu ya Rais jijini Dar es salaam itabaki kama Makumbusho.
“Hatuwezi kuuza ikulu, Ikulu itabaki pale kama makumbusho” Alisema Rais
Magufuli huku akishangiliwa na baadhi ya wanachama chama cha Mapinduzi.
Naye Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa amemhakikishia Rais kuwa
watatekeleza kwa ukamilifu maagizo yake ikiwa na pamoja na Mpango wa
serikali kuhamia Dodoma.
Kwa upande mwingine Rais Dkt. John Magufuli hivi karibuni alitangaza
kuuza majengo ya wizara Dar es Salaam, atakapohamia yeye katika makao
makuu ya nchi mkoani Dodoma.
Rais Magufuli alisema hayo hivi karibuni kwenye mkutano wa hadhara
mkoani Singida, katika siku ya kwanza ya ziara yake ambapo alisisitiza
kuwa atahakikisha anauza baadhi ya majengo hayo kwa mnada, ili wale
wasiotaka kuhama, wahame kwa lazima.
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni