Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na 
Mkewe Mama Janeth Magufuli pamoja na Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, 
Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin Ngonyani, Mbunge wa Sumve Richard
 Ndassa wakipiga makofi mara baada ya tukio la uwekaji wa Jiwe la Msingi
 la Ujenzi wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na Upanuzi 
wa barabara ya Mwanza-airport.
Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katikati 
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Mitambo itakayotumika katika ujenzi 
wa Daraja la waenda kwa miguu la Furahisha pamoja na upanuzi wa barabara
 ya Mwanza-airport.
Mtendaji
 Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS, Mhandisi Patrick Mfugale 
akitoa maelezo ya namna daraja la Furahisha litakavyokuwa mara baada ya 
kukamilika.
Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia 
maelfu wa Wakazi wa Mwanza na vitongoji vyake mara baada ya kuzindua 
ujenzi wa Daraja la Furahisha jijini Mwanza
Wanachi wakishangilia wakati Rais Dkt. Magufuli alipokuwa akihutubia.
Mwanamuziki
 Christian Bella akisalimiana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 Dkt. John Pombe Magufuli mara baada ya kutumbuiza katika uwanja wa 
Furahisha jijini Mwanza. 
Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin
 Ngonyani ,Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella, Mke wa Rais, Mama 
Janeth Magufuli pamoja na Mbunge wa Ilemela Angelina Mabula wakiomba dua
 kabla ya kuhutubia maelfu wa wakazi wa jiji la Mwanza.
Rais
 wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na  
Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Edwin
 Ngonyani, Waziri wa Kilimo Mhandisi Charles Tizeba na Mkuu wa Mkoa wa 
Mwanza John Mongela wakiimba Wimbo wa Taifa kabla ya kuhutubia maelfu ya
 wakazi wa jiji la Mwanza. PICHA NA IKULU.












Hakuna maoni:
Chapisha Maoni