Mizigo ikitolewa kwenye gari.
Aman Issaya wa taasisi hiyo akiwa na kiroba cha sukari akielekea eneo la makabidhiano.
Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign,
Mpelo Kapama, akiwa amebeba kiroba cha sukari wakati taasisi hiyo
ilipotoa msaada wa vyakula na vifaa vya shuleni kwa Kituo cha Yatima
Group Trust Fund cha Chamazi Temekie jijini Dar es Salaam leo.
Vifaa hivyo viwekwa sawa kabla ya kukabidhi.
Aman Issaya wa taasisi hiyo (kushoto), akimkabidhi Katibu Mkuu wa Kituo hicho, msaada huo. Kulia ni Mratibu wa Taasisi ya The Hope Campaign, Mpelo Kapama na Furaha Kapama.
Furaha Kapama (kushoto), akimkabidhi msaada Katibu Mkuu wa Kituo hicho, Fred George.
Mwezeshaji Mkuu wa Kampuni hiyo, John Amigo ambaye ni mwimbaji wa nyimbo za injili akiwa katika pozi.
Upendo Kapama akikabidhi msaada huo.
Thomas Anzuluni akimkabidhi Katibu wa kituo hicho, Fred George msaada wa mafuta ya kula.
Mwakilishi wa Taasisi ya The Hope
Campaign, Stela Mpelo (kushoto), akiwakabidhi vifaa vya shule watoto
Yatima wa Kituo cha Yatima Group Trust Fund cha Chamazi Temeke jijini
Dar es Salaam. Kutoka kulia ni Ofisa wa taasisi hiyo, Thomas Anzuluni na
Katibu wa kituo hicho, Fred George.
Aman Issaya wa
taasisi hiyo (kushoto), na Katibu Mkuu wa Kituo hicho wakiwa wameshika
mipira iliyotolewa na taasisi hiyo kwa watoto wa kituo hicho.
Hapa ni kikosi kamili cha taasisi hiyo kabla ya kukabidhi msaada huo.
Ni pozi la kukata na shoka na vipeperushi mkononi.
Na Dotto Mwaibale
Na Dotto Mwaibale
TAASISI ya The Hope Campaign imetoa
msaada wa vyakula na vifaa vya shuleni kwa Kituo cha Yatima Group Trust
Fund cha Chamazi Temeke jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari
wakati wa kukabidhi msaada huo kituoni hapo Dar es Salaam leo asubuhi ,
Mratibu wa Taasisi hiyo Mpelo Kapama alisema msaada huo umelenga
kuwasaidia watoto hao kwa ajili ya chakula na vifaa vya kusomea.
"Taasisi yetu kupitia kwa mwezeshaji
wetu mkuu John Amigo imejijengea utamaduni wa kusaidia makundi
mbalimbali yenye uhitaji kama watoto hao na kambi za ukimbizi na mara
nyingi tumekuwa tukisaidia kituo hiki" alisema Kapama.
Katibu wa Kituo hicho cha Yatima, Fred
George alisema ni muhimu kwa jamii kujitokeza kusaidia Yatima na
kuwafariji kama ilivyofanya taasisi hiyo.
Alisema kituo hicho chenye watoto zaidi
ya 150 kimekuwa na changamoto ya chakula, fedha za kuwalipa wafanyakazi
pamoja na ujenzi wa uzio kwa ajili ya usalama.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni