KASESELA AWASWEKA NDANI WALINZI WAWILI WA KAMPUNI YA ULINZI YA AMAZON KWA KUNYANYASA WANANCHI

Leo saa 3 na dakika 25 Usiku mkuu wa wilaya Mh Richard Kasesela alipokea wakina mama 3 wakiwa wanatetemeka kwa baridi, wakilalamika kumwagiwa maji walipokuwa wamekaa kwenye eneo la kusubiria wagonjwa walio lazwa hasa kwa wale walio toka mbali. 

Maji hayo yalimwagwa na walinzi wa kampuni ya Amazon ambao ndio wamepewa kandarasi ya ulinzi hospitali ya Rufaa ya Iringa.
Mkuu wa wilaya Iringa, Richard Kasesela alifika hospitali kujionea mwenyewe hali halisi, baadae pia akapata taarifa kuwa jana yake Mlinzi alimpiga mzee aliyekuwa ameleta chakula hospitali na kumwaga kwa mateke. 

Mkuu wa wilaya aliamuru mlinzi huyo na mwenzake wakamatwe pia mwenye kampuni afike kituo cha polisi haraka iwezekanavyo.
"Hali hii imeudhi sana hasa ukiona jinsi wakina mama walivyo nyanyasika wengine vyombo vyao na chakula kuroweshwa maji." alisema Mh Kasesela.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni